Mchezo wa ligi kuu ya vodacom kati ya Azam FC na Simba sasa utachezwa kati ya uwanja wa Taifa ama wa Azam uliopo Chamanzi badala ya Mkwakwani Tanga.
Mchezo huo ulipangwa kuchezwa kwenye uwanja wa Taifa hapo awali na kisha kuamishiwa Tanga kwenye uwanja wa Mkwakwani baada ya serikali kutangaza kuufungia uwanja wa taifa.
Mchezo huo utakaopigwa september 11 mwaka huu jijini Dar es salam katika uwanja wa Taifa kama kutakuwa na maafikiano mazuri kati ya Azam na Serikali, ama utachezwa kwenye uwanja wa Azam uliopo Chamanzi na hii ni kwa mujibu wa taarifa iliyowekwa kwenye ukarasa wa facebook wa Azam na moderator.
Thursday, September 8, 2011
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Maoni:
Post a Comment