Saturday, September 24, 2011

Ngassa mpe sekunde moja

Posted By: kj - 4:05 PM

Share

& Comment

KOCHA wa Azam, Sterwart Hall amesema hatishiki na hali ya mshambuliaji wake Mrisho Ngassa kutofunga bao hadi sasa kwa maelezo kuwa ana mchango mkubwa kwenye timu na anahitaji sekunde moja tu kusababisha madhara.


Mfungaji huyo bora wa msimu uliopita hajafunga bao katika mechi tano alizoichezea Azam msimu huu huku mashabiki wakidai kwamba umaarufu wake umepotea tofauti na alivyokuwa Yanga.


"Sina wasiwasi hata kidogo na Ngassa, kama kocha wake ninajua ni nini anachokifanya uwanjani na nimemuingiza akafanye nini. Hata kama mashabiki hawaoni inategemea na uelewa wao wa masuala hayo," alisema kocha huyo.


"Lakini Ngassa ni mchezaji wa sekunde, ana madhara makubwa kwa washambuliaji hahitaji muda mrefu uwanjani, ndio maana naamini ni mchezaji mzuri."


Ngassa amekuwa akilaumu kwamba anakamiwa na kusisitiza kuwa waamuzi wamekuwa na utata katika uamuzi wao.




mwanaspoti.co.tz

0 Maoni:

Post a Comment

Copyright © CHAMA LANGU NI AZAM FC™ is a registered trademark.

Designed by Templateism. Hosted on Blogger Platform.