Sunday, September 25, 2011

Kaly na matumaini katika mchezo dhidi ya shooting

Posted By: kj - 11:36 PM

Share

& Comment

Japokuwa kikosi cha Azam FC kinakabiliwa na majeruhi wachezaji waliobaki wapo katika hari nzuri kucheza mchezo wa kesho dhidi ya Ruvu Shooting utakaochezwa kwenye uwanja wa Mlandizi mkoani Pwani.

Wachezaji wa Azam FC, Kipre Tchetche, Jamal Mnyate, Wahab Yahya na Obren Cuckovic wanasumbuliwa na majereha huku wachezaji Haji Nuhu na Abdulghan Gulam wapo katika mazoezi mepesi kwa ajili ya kujiweka vizuri kutokana na kusumbuliwa na majeraha ya muda mrefu.

Kocha msaidizi wa Azam FC, Kali Ongala ameiambia tovuti ya www.azamfc.co.tz kuwa timu ina wachezaji wengi kila nafasi hivyo kuwakosa wachezaji hao haimaanishi kwamba itafanya vibaya bali nafasi zao zitachukuliwa na wachezaji wengine.

“Tunashukuru tulifanya usajili makini, tukiwa na majeruhi nafasi zao zinatumiwa na wachezaji wengine waliopo katika kikosi, timu ni ya wachezaji wengi na sio mchezaji mmoja,” alisema Kali.

Kali aliongeza kuwa maandalizi ya mechi ya kesho na mechi zingine yapo katika hali nzuri, wachezaji wote wapo kambini na wanafanya mazoezi ya nguvu na yakutosha kuhimili mchezo wowote.

Wakiwa mazoezini jana mchezaji Waziri Salum alipata majeraha mguuni, huku golikipa Obren Curcovic alifanya mazoezi ya peke yake kutokana na kusumbuliwa na matatizo madogo kwenye kidole.

Azam FC itashuka uwanjani Mlandizi ikiwa na pointi 14 huku wakiwa na rekodi ya kushinda michezo mitatu mfulizo, ikiwa na sare mbili, ilishinda mchezo wa kwanza na kufungwa mchezo wa pili.

Baada ya mchezo wa kesho kikosi cha Azam FC kitapumzika kwa muda wa wiki mbili kupisha maandalizi ya timu ya Taifa ‘Taifa Stars’ inaojiandaa kucheza mchezo dhidi ya timu ya taifa ya Morocco utakaochezwa Oct 9 nchini Morocco, mchezo unakamilisha ratiba ya kuwania kufuzu kucheza fainali za Afrika februari mwaka kesho.


www.azamfc.co.tz

0 Maoni:

Post a Comment

Copyright © CHAMA LANGU NI AZAM FC™ is a registered trademark.

Designed by Templateism. Hosted on Blogger Platform.