Saturday, September 17, 2011

REDONDO USHINDI LAZIMA

Posted By: kj - 6:13 PM

Share

& Comment

Kiungo Ramadhani Chombo ‘Redondo’ amewatoa hofu mashabiki wa Azam FC kwa kuwa hakikishia ushindi katika mechi zijazo za ligi kuu ukiwepo mchezo wa kesho dhidi ya Yanga utakaochezwa kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na tovuti ya www.azamfc.co.tz Redondo amesema wamefanya maandalizi ya kutosha kupambana na timu yoyote watakayokutana nayo.

“Timu ina hari nzuri na arikubwa, kwa kuwa tumekuwa pamoja muda mrefu, tunahitaji ushindi kwa kila mechi tunayokutana nayo ili kufikia malengo yetu, hata kama ni Yanga kwetu ushindi lazima” alisema Redondo.

Redondo ameongeza kuwa baada ya kucheza michezo iliyopita, timu inapigana kadri iwezavyo ili kukaa katika nafasi nzuri. Naye nahodha msaidizi wa timu hiyo, Aggrey Morris amesema wapo katika maandalizi mazuri na mechi dhidi ya Yanga ni sawa na mechi ya kawaida hivyo ushindi utapatikana.

Amesema wapenzi wa Azam FC wasiwe na mashaka, wachezaji wote wapo makini na wajitokeze kwa wingi kwani hawatawaangusha.

Kocha mkuu Stewart Hall amezungumzia mchezo huo kama ni moja ya mechi muhimu kwao ya kupata pointi tatu, kwakuamini kuwa kutokana na wachezaji kuonyesha hali ya kupatikana kwa ushindi.

“Wachezaji wapo kamili, MrishoNgassa na Salum Aboubakar ‘Sure Boy’ wameshamaliza adhabu zao hivyo watakuwepo katika mchezo huo” alisema Stewart.

Ameongeza kuwa watatumia mapungufu walionayo Yanga kupata ushindi, anaamini safu yake ya ulinzi iliyoko chini ya nahodha Aggrey Morris watahakikisha hakuna madhara katika lango lao litakalosimamiwa na makipa Mwadini Ally na Obren Cuckovic.

Azam FC kesho itacheza mchezo wake wa saba wa ligi kuu dhidi ya Yanga, Azam itashuka katika mchezo huo ikiwa na pointi nane, ikishinda michezo miwili, sare michezo miwili na kupoteza mchezo mmoja, wakati Yanga inapointi 6.



azamfc.co.tz

0 Maoni:

Post a Comment

Copyright © CHAMA LANGU NI AZAM FC™ is a registered trademark.

Designed by Templateism. Hosted on Blogger Platform.