Monday, September 26, 2011

REFA ATOKA NA MAGOLI YA AZAM NA KUWAPA POINT MOJA

Posted By: kj - 7:20 PM

Share

& Comment

Refa ametoka na magoli ya Azam ilikuwa kauli ya Moderator wa ukurasa wa Azam FC ndani ya facebook akiwa anafafanua kilicho jiri katika mchezo wa leo uliokwisha sare ya bila kufungana.

Azam walikuwa wageni wa Ruvu shooting katika uwanja wa Mabatini mkoani Pwani, ambapo mchezo ulio kwisha kwa sare ya bila kufungana.

Azam FC walidumbukiza mpira kimiani mara kadhaa ambapo refa aliyakataa magoli hayo. Moja ya goli lililo kataliwa ni shuti la Mrisho Ngassa la mita 18 ambapo refa aliamuru kuwa mfungaji alikuwa kaotea.

Kwa matokeo hayo Azam FC wanasalai katika nafasi ya pili katika msimamo wa kiwa na point 15 wakiwa nyuma kwa point 3 kwa Simba anae ongoza ligi.

0 Maoni:

Post a Comment

Copyright © CHAMA LANGU NI AZAM FC™ is a registered trademark.

Designed by Templateism. Hosted on Blogger Platform.