nukuu toka mwanaspoti.
Kocha Muingereza Stewart Hall ameomba mamilioni mengine ya pesa kwa uongozi ya kufanya usajili kwenye dirisha dogo Desemba.
Hall alisema; "Timu mpaka sasa imecheza vizuri tupo kwenye mwenendo mzuri nina ukuta imara na makipa wawili wazuri sana. Lakini nimeona baadhi ya dosari ambazo tayari nimeshazungumza na wenzangu kwenye benchi pamoja na uongozi."
"Nimewaambia viongozi kwamba nahitaji fedha kwa ajili ya usajili wa kurekebisha mapengo machache niliyokwisha yaona hadi sasa, tumekubaliana katika hilo na wakati ukifika tutasajili wachezaji katika nafasi, ni mapema sana kuzitaja kwa sasa.
"Hata idadi bado siwezi kuiweka hadharani lakini, kuna baadhi tutawatoa kwa mkopo. Lengo ni kuhakikisha kwamba timu inakuwa imara zaidi na kujiweka katika nafasi nzuri ya kushindania ubingwa wa Tanzania Bara kwavile kila kitu kinawezekana,"alisema kocha huyo ambaye timu yake ndiyo imesajili kwa gharama kubwa zaidi kabla ya kuanza kwa Ligi Kuu.
Timu hiyo ina mastaa kutoka Serbia, Ghana, Ivory Coast, Kenya na Tanzania na imekuwa tishio kubwa kwa Simba na Yanga.
Wikichache zilizopita ilitoka suluhu na Simba kabla ya kuipiga Yanga bao 1-0 Jumapili iliyopita.
Kutoka kwa Aboodmsuni Na Soka La Bongo anaripoti kuwa, Beki toka Uganda aliyetamba na Simba katika rekodi ya timu hiyo kucheza bila kufungwa msimu wa 2009/10, Joseph Owino Gere amemwaga wino wa kuitumikia azam FC.
soma zaidi
Tuesday, September 20, 2011
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Maoni:
Post a Comment