Baada ya kunyimwa magoli yake katika mchezo wake wa 6 kuichezea Azam FC msimu huu, Mrisho Khalfan Ngassa leo katika mchezo wake wa 7 amefanikiwa kutoka na goli pale Azam FC walipo karibishwa na JKT Ruvu katika uwanja wa Azam.
Ngassa msimu uliopita alianza kutikisa nyavu katika mchezo wake wa 6 na kuibuka mfungaji bora katika msimu huo, na msimu huu ameanza kutikisa nyavu katika mchezo wa 7 wa leo.
Katika mchezo wa leo Azam FC walipata goli la kuongoza katika dakika ya kwanza ya mchezo kupitia kwa Mrisho Ngassa na goli la pili lilifungwa na mshambuliaji hatari nchini John Raphael Bocco katika dakika ya 89 na kufikisha goli la 6 ndani ya mechi 9 alizocheza.
Kwa ushindi huo wa goli 2-0 walioupata Azam mbele ya JKT Ruvu ulimshuhudia Abdulhalim Humoud akianza katika nafasi ya kiungo na kuifanya Azam FC kufikisha point 18.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Maoni:
Post a Comment