Saturday, November 26, 2011
Academy washindwa kurejesha kombe nyumbani
Posted By: kj - 12:23 PMAzam Academy iliyokuwa inaundwa na wachezaji chini ya miaka 17 na bila ya nyota wao wa 5 wameshindwa kulirejesha kombe la uhai nyumbani, baada ya kufungwa kwa mikwaju ya penati 4-5 na Simba SC.
Mchezo huo uliochezwa katika uwanja wa Karume Saa 3 asubuhi baina ya Simba na mabingwa mara mbili Azam Academy ulizishuhudia timu hizo zikimaliza dakika 120 bila kufungana.
Simba wamefanikiwa kulitwaa kombe hilo linalo dhaminiwa na Kampuni inayomiliki timu ya Azam FC Bakhresa kupitia kinywaji cha Uhai, huku wakifanikiwa kulipa kisasa kwa Azam Academy ambayo iliwavua ubingwa wa michuano ya vijana iliyoandaliwa na kituo cha Rolling Stone Mkoani Arusha.
Mshambuliaji wa Azam FC, Simon Happygod Msuva ameibuka mfungaji bora na golikipa wa Azam, Aishi Mfula amekuwa golikipa bora wa mashindano. Huku Serengeti Boys ambayo inawachezaji wa 5 wakutumainiwa wa Azam Academy wakichukuwa nafasi ya 3.
Michuano hiyo iliyofanyika kwa mara ya nne kukishuhudi Simba na Ruvu Shooting wakitwa kombe hilo mara moja moja kwa kila timu huku Azam Academy wamelitwaa mara mbili.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)

SIB 90
POPULAR
TAGS
0 Maoni:
Post a Comment