Tuesday, November 29, 2011

Azam yatoa 10 kwa mkopo, yupo Redondo

Posted By: kj - 8:45 AM

Share

& Comment

Kiuongo wa Azam FC pamoja na Timu ya Taifa Ramadhan Chombo Redondo ametolewa kwa mkopo kwenda Moro United. Huku kiuongo wa Azam Academy Ibrahim Rajab Jeba akipelekwa Villa squad kwa mkopo.

Kwa mujibu wa Taarifa iliyowekwa katika ukurasa wa Azam FC ndani ya Facebook inasema klabu hiyo yenye maskani yake Chamanzi imewatoa wachezaji 10 kwa mkopo huku wawili wakiwa wanatoka katika timu kubwa na wengine 8 wakitoka katika Azam Academy katika vilabu vya Villa squad, Moro united na JKT Oljoro.

"Wakati dirisha dogo likielekea kufungwa, Azam FC iimewapeleka kwa mkopo Villa Squad wachezaji watano, wanne wakitoka Azam U-20 Fred Cosmas, Daudi Mwasongwe, Ibrahim Rajab, Adam Gambo na Malika Philip. Moro United imechukua kwa mkopo wanne Wandwi na Msuva toka U-20 na Redondo na Mnyate toka timu ya wakubwa na JKT Oljoro imemuazima Omary Mtaki," ilieleza Taarifa hiyo.

0 Maoni:

Post a Comment

Copyright © CHAMA LANGU NI AZAM FC™ is a registered trademark.

Designed by Templateism. Hosted on Blogger Platform.