Tuesday, November 29, 2011

Babi atua AZAM FC

Posted By: kj - 2:47 PM

Share

& Comment


KOCHA wa Yanga, Kostadin Papic alionyesha nia lakini Azam FC imemuonyesha njia ya kurudia nyumbani kiungo wa Taifa Stars, Abdi Kassim Babi.

Kwa maneno mengine, Azam FC imempiga bao kweupe Papic, ambaye ndio kocha wa kwanza aliyeonyesha kumhitaji Babi. Wito wa Papic uliokaririwa na gazeti la Mwanaspoti ni kama uliwaamsha usingizini Azam FC, ambao walitumia mbinu za medani na kuizunguka Yanga na kumnasa Babi, ambaye alikuwa akicheza soka ya kulipwa Vietnam.

Mtego wa Azam FC haujamnasa Babi pekee, pia wamemvuta staa kutoka Ivory Coast, Kipre Bolou.

Kumbuka Bolou ni pacha wa mshambuliaji mwingine wa Azam FC, Kipre Tchetche.

Wakali hao walianguka saini zao kwenye makao makuu ya Azam FC jana Jumatatu yaliyoko Dar es Salaam. Walifanyiwa uchunguzi wa afya mapema katika hospitali ya AAR.

Babi, alikuwa akicheza soka ya kulipwa nchini Vietnam katika klabu ya Dong Tam Long An ambayo sasa imeshuka daraja na itacheza Ligi Daraja la kwanza msimu ujao.

Bolou anatokea Sewe inayoshiriki Ligi Kuu ya Ivory Coast na ilishika nafasi ya tatu katika ligi hiyo. Nyota hao wanaungana na Mganda Joseph Owino pamoja na Gaudence Mwaikimba, ambao pia wamesaini katika kipindi hiki cha dirisha dogo.

Akizungumza na Mwanaspoti, Katibu Mkuu wa Azam FC, Idrissa Nassor alisema: "Wachezaji hao tayari tumemalizana na wataanza kuitumikia Azam FC katika mzunguko wa pili wa ligi. Babi tumevunja mkataba wake na Dong Tam Long An, tumemsainisha mkataba wa miezi 18 tayari, wakati Kipre Bolou amesaini mkataba wa mwaka mmoja," alisema Nassor.

Babi aliiambia Mwanaspoti ametua Azam FC kwa kuzingatia maslahi. Nimesaini mkataba na Azam FC kwani wamevunja mkataba na timu yangu ya Vietnam," alisema Babi, ambaye amegoma kutaja dau ambalo wamemng'oa huko.

Kwa upande wake, Bolou, ambaye ni mshambuliaji, alisema "amefurahia kuja kucheza Tanzania na kuungana na ndugu yake. Nitajitolea kwa nguvu zangu zote kuhakikisha nafanya vizuri na Azam FC," alisema Bolou, ambaye alikuwemo katika kikosi cha Ivory Coast kilichocheza Kombe la Chalenji mwaka jana.


Mwanaspoti

0 Maoni:

Post a Comment

Copyright © CHAMA LANGU NI AZAM FC™ is a registered trademark.

Designed by Templateism. Hosted on Blogger Platform.