Natumai mashabiki wote wa Azam FC hamjambo na mnaendelea vyema na pilika pilika za hapa na pale, na penda kuwapongeza Azam Academy kwa kutinga Hatua ya Fainali kwa mara ya 3 ya Uhai Cup.
Tuliitisha kikao hapo agust 13 lakini hakikuweza kufanyika baada ya kujikuta viongozi watupu katika kikao hicho, ambacho kingekuja na mipango mipya kwa club hii ya Mashabiki wa Azam FC kuanzia utaratibu wa kadi mpaka katiba.
Tunajiandaa kuutisha kikao kingine hapo January 12 mwakani, siku ya Mapinduzi ya Zanzibar, lakini kitakuwepo endapo tutapata wadau si chini ya 50 mpaka december 30 ambao watakuwa teyari kuhudhuria kikao hicho ambacho kitakuwa na agenda zilezile za kikao kilichopita.
Kwa wale waliokuwa wanauliza kadi ya kuwa mmoja wa mwanachama wa mashabiki wa Azam FC, jawabu litapatikana katika kikao hicho kitakacho fanyika january 12 mwakani.
Kwa walewote watakao kuwa teyari kushiriki kikao hicho tutaarifu kupitia azamfan@hotmail.com, vile vile katika kututumia, ambatanisha jina lako kamili.
December 30 saa 5 usiku tutapitia hiyo email address kupata idadi ya watu waliyoteyari kushiriki kikao hicho, na January 1, siku ya mwaka mpya tutakuja na taarifa kama kikao kitakuwepo ama la, na kama kipo, kitafanyika sehemu gani.
NB: Ukipata taarifa hii watangazie mashabiki wenzako, kwa pamoja Tunatumia Bidhaa Bora, tukishabikia Timu Bora.
Thursday, November 24, 2011
Subscribe to:
Post Comments (Atom)

SIB 90
POPULAR
TAGS
0 Maoni:
Post a Comment