Thursday, November 24, 2011

Azam yasajili Pacha wa Kipre Tchetche

Posted By: kj - 10:21 PM

Share

& Comment

Baada ya kuwaacha Waghana wawili na kumsajili beki toka Uganda Joseph Owino, sasa Azam FC wamepiga hodi Ivory coast na kumsajili pacha Kipre Tchetche, Kipre Bolou kujaza nafasi ya Waghana.

Kwa mujibu wa taarifa zilizowekwa kwenye kurasa ya Azam katika Facebook inasema: "Azam FC imemsajili Kipre Bolou Michael ambaye ni pacha wa Kipre Tchetche....Bolou na Nduguye Tchetche watatua nchini Jumapili hii Novemba 27."

Bolou anakamilisha idadi ya wachezaji wakigeni watano ndani ya Azam FC ambao ni Ibrahim Shikanda (Kenya), Joseph Owino (Uganda), Obren Circovic (Serbia), Kipre Tchetche na Kipre Bolou toka Ivory coast.

Katika dirisha dogo hili Azam FC wamesajili wachezaji watatu na kuwaacha wawili ambao ni Waghana Afiu na Wahab. Ambapo walio ongezwa ni Gaudence Mwaikimba, Joseph Owino pamoja na Kipre Bolou.

0 Maoni:

Post a Comment

Copyright © CHAMA LANGU NI AZAM FC™ is a registered trademark.

Designed by Templateism. Hosted on Blogger Platform.