Friday, November 25, 2011
Mnyate apelekwa kwa mkopo Moro
Posted By: kj - 6:58 AMKLABU ya Azam FC ya jijini Dar es Salaam, imemtoa kwa mkopo winga wake, Jamal Mnyate ambaye sasa atavaa jezi ya Moro United duru la pili Ligi Kuu Januari mwakani.
Afisa Habari wa Azam, Jafari Iddi alithibitisha jana taarifa za mchezaji huyo kwenda Moro United.
“Tumefanya mazunguzo na Moro United na mchezaji mwenyewe, hivyo Jamal Mnyate ataichezea Moro Utd mzunguko wa pili,” alisema Iddi.
“Mnyate (Jamal) ni mchezaji mzuri, umri wake bado unamruhusu kucheza soka, tumeona kukaa naye pasipo kumtumia ni sawa na kukiua kipaji chake,” aliongeza.
“Tunaamini kutua kwake Moro atapata nafasi ya kucheza kikosi cha kwanza nakuendelea kupata uzoefu zaidi,” alisisitiza.
Iddi alisema kumtoa mchezaji huyo kwa mkopo haina maana hawamuhitaji, isipokuwa kiwango chake kitazidi kuimarika zaidi watamrejesha kundini.
Kikwazo kwa yosso huyo kutolewa kwa mkopo nikucheza namba moja na nyota Kipre Tchetche, Mrisho Ngassa na Mcha Khamis.
Naye, katibu wa Moro United, Hamza Abdallah alikiri timu yake kufikia makubaliano na mchezaji huyo kwenda kuchezea timu yao.
Mnyate amekuwa mchezaji wa tatu kutolewa kwa mkopo na Azam, akiwafuata Seleman Kassim ‘Selembe’ na Sino Agustino waliokwenda African Lyon.
Mwananchi
Subscribe to:
Post Comments (Atom)

SIB 90
POPULAR
TAGS
0 Maoni:
Post a Comment