Sunday, January 29, 2012

Azam kuwa mgeni wa Moro united Chamanzi kesho

Posted By: azam fans - 10:46 PM

Share

& Comment


Mabingwa wa Mapinduzi Azam FC wanateremka uwanjani hapo kesho wakiwa wageni wa Moro united katika uwanja wa Azam uliopo Chamanzi.

Mkosi huo wa Azam hapo kesho utamkosa beki Erasto Nyoni ambaye ameelekea Iringa kwenye Msiba wa Mamaake uliotokea jana, lakini nafasi yake itazibwa vyema Mkenya Ibrahim Shikanda katika mchezo wa pili wa duru la pili ligi kuu ya vodacom.

Moro united ni timu nzuri inayoundwa na vijana ambao waliisumbua yanga katika mchezo wa awali uliochezwa Taifa, hivyo mchezo wa kesho unatarajiwa kuwa wa ushindani.

Kiingilio cha mchezo huo ni Tsh 3000 kwa mzunguko na Tsh 10,000 kwa jukwaa kuu.

0 Maoni:

Post a Comment

Copyright © 2025 CHAMA LANGU NI AZAM FC™ is a registered trademark.

Designed by Templateism. Hosted on Blogger Platform.