Wednesday, January 25, 2012
Azam wafungua duru la pili kwa ushindi
Posted By: kj - 7:33 PMMabingwa wa mapinduzi Cup wameanza salama safari ya duru la pili la kusaka ubingwa wa Tanzania Bara, baada ya kuwachapa goli 2-1 African lyon.
Azam FC walianza safari yao kwa goli la kujifunga Lyon na baadae kidogo Lyon kusawazisha goli hilo kupitia kwa Semi Kessi.
Azam ambao wanasifika kwa pasi nyingi walipata goli la pili kupitia kwa Mfungaji bora wa wakati wote wa Azam John Bocco Adbayor aliyefunga goli lake la 8 msimu huu.
Azam FC watarejea uwanjani tena jumapili january 29 dhidi ya Moro united, na sasa wako katika nafasi ya 3 wakiwa na point 26 nyuma kwa point 2 kwa Yanga na point 5 kwa kinara Simba SC.
What's Related?
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Maoni:
Post a Comment