Friday, January 27, 2012
Twiga wasogeza mbele mchezo wa Azam
Posted By: azam fans - 3:51 PMMchezo wa kusaka tiketi ya kushiriki mataifa ya Africa kwa soka la wanawake kati ya Tanzania (Twiga Stars) na Namibia utakao chezwa jumapili katika uwanja wa Taifa umeisogeza mbele siku moja mchezo wa Azam FC dhidi ya Moro united.
Azam FC na Moro United walitarajiwa kucheza jumapili ya january 29 katika uwanja wa Azam, umesogezwa mbele mpaka january 30 mwaka huu na utapigwa katika uwanja wa Azam uliopo Chamanzi, nnje ya jiji la Dar es salaam.
Mchezo huo umesogezwa mbele ili kuwapa nafasi mashabiki wa Azam kwenda kuhudhuria mchezo huo wa Twiga Stars na Namibia, kitu ambacho hapo awali ulikuwa unawaacha njia panda mashabiki wa Azam wa wapi pakwenda kati ya Azam Stadium ama Taifa.
What's Related?
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Maoni:
Post a Comment