Wednesday, January 4, 2012

Mwaikimba aiokoa Azam FC

Posted By: kj - 7:47 PM

Share

& Comment


Mshambuliaji mpya wa Azam FC, Gaudence Mwaikimba ameipatia point moja timu ya Azam FC pale walipo wakabili Mafunzo FC walio wafunza Soka Yanga.

Katika mchezo huo uliochezwa katika uwanja Amani, Mafunzo FC walikuwa wa mwanzo kupata goli katika dakika ya 12 kabla ya Mwaikimba kuisawazishia Azam FC.

Katika mchezo huo ulishuhudia urejeo wa Mrisho Khalfan Ngassa katika kikosi kufuatia jeraha alilolipata pale Azam FC walipocheza na Yanga mwaka jana katika mchezo wa kirafiki.

Azam FC inayoongoza Kundi B kwa kuwa na point 4 watawavaa Yanga siku ya ijumaa, katika mchezo wa mwisho wa makundi katika michuano hiyo ya mapinduzi.

0 Maoni:

Post a Comment

Copyright © CHAMA LANGU NI AZAM FC™ is a registered trademark.

Designed by Templateism. Hosted on Blogger Platform.