Wednesday, February 22, 2012
Azam waendelea na mazoezi
Posted By: kj - 1:33 PMTimu ya Azam FC imeendelea na mazoezi kujega mwili na mbinu ikiwa ni maandalizi kwa ajili ya mechi zilizobaki za ligi kuu.
Mazoezi yamefanyika katika uwanja wa Azam Chamazi jijini Dar es Salaam kujumuisha wachezaji wote isipokuwa wale walioitwa timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars'.
Wakiwa katika mazoezi hayo beki Joseph Owino alijumuika na kikosi hicho kwa mazoezi ya kuimarisha mwili 'fitness', huku mchezaji Abdulghan Gulam akifanya mazoezi na timu ndogo kutokana na kupona jeraha la mguuni.
Wachezaji wengine walifanya mazoezi yote mbinu na kuimarisha mwili Gym kwa muda wa masaa mawili na nusu, Gulam ataanza mazoezi na kikosi hicho kesho asubuhi.
Akielezea umuhimu wa mazoezi hayo kocha Stewart Hall amesema kwa kipindi hiki wanatakiwa kufanya mazoezi hayo kwa kuwa hakuna mechi karibuni hivyo miili yao inatakiwa ijengeke zaidi.
Alisema wakifanya mazoezi hiyo kwa muda wa wiki mbili watakuwa na miili imara itakayowasaidia kumalizia vyema mechi za ligi kuu zilizobaki.
Stewart aliongeza kuwa wachezaji watafanya mazoezi ya aina hiyo kwa wiki mbili na kuendelea na mazoezi ya kawaida kwa ajili ya mechi.
Kocha amesema siku ya Alhamis ya wiki hii atasafiri kuelekea nchini Uingereza kusalimia familia yake, wakati huo timu itakuwa chini ya kocha wa Azam Academy, Vivek Nagul akishirikiana na kocha msaidizi Kaly Ongala.
Stewart atarejea nchini Machi 1, na kufanya mazoezi na timu Machi 2 kabla ya kuweka kambi Machi 3 kwa ajili ya mechi dhidi ya Coastal Union itakayochezwa Machi 7 kwenye uwanja huohuo.
Wachezaji waliohudhuria mazoezini ni golikipa Aishi Mfula, Erasto Nyoni, Abdulhalim Humud, Said Morad, Michael na Tchetche Kipre, Ibrahim Shikanda, Zahor Pazi, Hamis Mcha, Ibrahim Mwaipopo, Himid Mao, Ghulam Abdallah, na Joseph Owino.
Jabir Aziz hakuudhuria mazoezini kutokana na kusumbuliwa na maumivu ya tumbo, wachezaji walioitwa timu ya taifa ni Mwadini Ally, Agrey Morris, Salum Aboubakar, John Bocco, Mrisho Ngasa, Waziri Salum na Abdi Kassim.
azamfc.co.tz
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Maoni:
Post a Comment