Madada wakiishangilia Azam kwa nguvu
Tumaini jipya la Arusha JKT Oljoro wameukabili mziki wa Azam FC baada ya kulishwa viloba vitatu vya Sembe ya Azam katika uwanja wa Azam.
Mchezo huo wa ligi kuu ya vodacom uliotawaliwa vyema na kiungo Salum Abubakari Sure Boy, huku nao JKT Oljoro wakipoteza baadhi ya nafasi ya kujipatia magoli hii leo.
Katika dakika ya 12 ya mchezo JKT Oljoro walifunga bao lililo kataliwa na waamuzi, na kupelekea Azam FC kuongeza kasi ya mchezo na mnamo dakika ya 22 John Bocco alifungua ukurasa wa magoli kwa kufunga goli lake la 11.
Goli hilo lilitokana na pasi safi ya kuuchop mpira toka kwa kiungo mchezeshaji aliyeonekana kucheza upande wa kushoto kwenye makaratasi Sure Boy.
Kabla JKT Oljoro hawajakaa sawa Mrisho Khalfani Ngassa aliifungia Azam FC goli la pili akipokea pasi safi toka kwa kiungo mwenye mashuti makali Abdi Kassim Babi katika dakika ya 26, na kupelekea Azam kwenda mapumziko wakiwa mbele goli 2.
Kipindi cha pili kilianza kwa JKT Oljoro kuliandama goli la Azam FC na walitumia takribani Dakika 10 wakicheza zaidi langoni mwa Azam FC bila mafanikio ya kumchukulia Mwadini.
Katika dakika ya 55 mpira ulipigwa mrefu golini la Oljoro na beki wa Oljoro alipewa presha na Bocco na kupelekea kupiga pasi kwa kipa wake ambaye naye alipewa presha na Bocco hivyo kupelekea kutoa pasi mkaa kwa Abdi Kassim Babi na bila kufanya ajizi aliifungia Azam goli la tatu.
Baada ya goli hilo Azam FC waliokuwa wanashangiliwa kwa nguvu na madada, huku wakizomewa na mashabiki A Simba na Yanga waliojitokeza uwanjani hapo kushuhudia Burudani ya soka inayopatikana Chamanzi pekee katika soka la bongo walicheza kwa kuonana huku Abdul Halim Homoud na kupelekea mchezo kumalizika kwa Azam kuibuka ushindi wa goli 3-0 na kufikisha point 32 wakishika nafasi ya pili katika msimamo wa ligi.
0 Maoni:
Post a Comment