Friday, February 17, 2012

Taifa stars yasogeza mbele mpambano wa Azam na Yanga

Posted By: kj - 2:56 PM

Share

& Comment


Timu ya Taifa ya Tanzania Taifa Stars imesogeza mbele mchezo kati ya Azam FC na Yanga uliokuwa uchezwe february 22 katika uwanja wa Taifa na sasa utachezwa machi 10.

Taifa Stars wanatarajiwa kuingia kambini february 20 kujianda na mchezo wa kirafiki dhidi DR Congo na mchezo wa kufuzu mataifa ya Africa dhidi ya Msumbiji.

Taarifa toka katika shirikisho la Soka nchini TFF, inaonyesha kuwa mchezo namba 132 kati ya Azam na Yanga utapigwa machi 10, badala ya february 22 mwaka huu.

"Tarehe mpya za mechi husika na namba zake ni kama ifuatavyo; mechi namba 131 kati ya JKT Ruvu na Toto Africans sasa itachezwa Machi 3 mwaka huu, mechi namba 132 kati ya Yanga na Azam (Machi 10 mwaka huu), mechi namba 133 kati ya JKT Oljoro na Kagera Sugar (Machi 3 mwaka huu)," ilieleza taarifa ya ofisa habari wa TFF Boniface Wambura.

Katika hatua nyingine kocha wa Taifa Stars Jan Poulsein amemuita kwa mara ya kwanza kiungo mchezeshaji wa Azam Salum Abubakari 'Sure Boy' kwa ajili ya mpambano dhidi ya DR Congo february 23 na february 29 dhidi ya Msumbiji.

Wachezaji wengine wa Azam walioitwa kuunda kikosi cha wachezaji 23 ni pamoja na kipa Mwadini Ali, Aggrey Morris, Abdi Kassim, John Bocco na Mrisho Ngasa.

0 Maoni:

Post a Comment

Copyright © CHAMA LANGU NI AZAM FC™ is a registered trademark.

Designed by Templateism. Hosted on Blogger Platform.