Ajax Cape Town ya Afrika ya Kusini, Ajax ambayo ilianzishwa mwaka 1999 kwa muunganiko wa klabu za Merger of Seven Stars na Cape Town Spurs ambayo iliwaibua nyota wanaotamba duniani kama Steven Piennar, na Obi Mikel hivi sasa ni moja kati ya timu zenye kutazamwa kama kiini cha uzalishaji wa timu ya taifa ya nchi hiyo, pia timu hiyo imekuwa ikipata nafasi ya kucheza michuano ya CAF.
Azam FC ambao lengo lao kubwa ni kutwaa ubingwa na kutinga katika michuano ya Afrika msimu huu, imeonesha mwanga na hivi sasa ina wachezaji wengi ambao wanaichezea timu ya taifa. Uwezo mdogo wa kiuzohefu unafunikwa na mafanikio ya klabu hiyo kucheza kama timu isiyo na staa, Azam wanacheza kwa ushirikiano mzuri na wachezaji wake wanacheza kwa viwango bora kama timu moja, ambayo inafanya kazi kwa pamoja. Baada ya misimu mitatu ya kumaliza katika nafasi ya tatu sasa “Wana lamba lamba” hao wanasaka taji la kwanza la ligi kuu, Bara. Hivi sasa wapo pointi sawa na Simba katika kilele cha uongozi katika ligi kuu.
IMETOKEA WAPI TIMU HII?
“Wafanyakazi wa moja ya viwanda waliamua kuanzisha timu hii kwa blengo la kujifurahisha mwaka 2004. Ikiitwa Mzizima FC . Mwaka 2005 tuliamua kuisajili na kushiriki katika ligi daraja la tatu, na tukafanikiwa kuwa mabingwa wa Mkoa wa kisoka, Ilala.” Anasema kocha msaidizi wa zamani wa klabu hiyo Mohammed Seif King. “Msimu wa mwaka 2006 wakati tukiwa katika maandalizi ya ligi daraja la pili TFF ikafuta ligi za madaraja, kuanzishwa hii ligi ya TFF kuanzia ngazi ya wilaya. Mwaka 2007 hatukufanya vizuri, nkatika ligi hiyo ya TFF, hapo ndipo tukamuomba Kurugenzi atusaidie katika kutafuta wachezaji wenye uwezo na kuwagharamikia ili tupate nafasi ya kucheza ligi kuu” anaeleza kocha huyo ambaye alikuwa ni miongoni mwa waanzilishi wa kwanza wa Azam FC.
JUlai, 27 mwaka 2008 baada ya ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Majimaji kwenye uwanja wa Jamhuri, Dodoma, Azam FC ikapanda daraja na kuwa miongoni mwa timu za ligi kuu. Kwa sasa Azam ni moja ya timu nne zenye nguvu nchini, na wamekuwa washindani wa kuwania ubingwa kwa msimu wa tatu sasa, uku tangu wapande daraja wamemaliza katika nafasi ya tatu mara tatu. Azam ambayo ilipandishwa daraja na wachezaji nyota waliotamba miaka ya nyuma kama Suleiman Matola, Shekhan Rashid, Kamba Lufo, Boniface Pawassa, Steven Nyenge, Salehe Hilal na wengineo inaweza kufikia matarajio yao hayo kama wachezaji wa sasa wataweka nia nia kwa dhati na kufanya kazi uwanjani. WAkifaidikika na uwepo wa Mwalimu wa kigeni kutoka nchini England, Stewart Hall, Azam FC hivi sasa timu hii inanufaika na uwepo wa vifaa vya kisasa, uwanja wa kisasa, zaidi ni kwamba wanaingiza pesa nyingi. “Walimu wa kigeni wana faida kubwa sana nchi kwani kila ambacho wamekuwa wakihitaji hupatiwa, tofauti na walimu wazawa ambao ni mara chache husikilizwa na kutimiziwa vitu muhimu anavyokuwa akihitaji, nakumbuka kuwa sisi wakati tunapandisha timu tulikabiliwa na changamoto nyingi, hasa kwenye masuala ya uhitaji wa vifaa, na mambo mengine muhimu, nakumbuka tulikuwa tukienda uwanjani tunapata katoni mbili tu za maji, lakini tazama sasa wanapata kila kitu, hiyo ni sababu moja wanayotakiwa wawe makini na kufanya kazi uwanjani, mana ubingwa hauji kwa kuongea katika vyombo vya habari. WAtambue kuwa kuna timu nyingine tatu ukitoa wao zina uwezo wa kutwaa ubingwa huo hivyo ni lazima wafanye kazi” anasema Mohammed Seif King ambaye alikuwa mukusanya “data” wa Neidor Dos Santos wakati alipokuwa kocha wa Azam na Itamor Amourin.
Wengi waichukulia Azam kama timu ambayo haitaweza kupambana na nguvu ya klabu kubwa za Simba na Yanga. Kwani timu kama Moro United ilishindwa kufanya hivyo katikati ya miaka ya 2000, Moro iliyokuwa na mkusanyiko wa wachezaji nyota nchini na Afrika Mashariki kwa ujumla , ilikuwa pesa, na uwezo mzuri ndani ya uwanja, wakamaliza raundi nya kwanza kwa tofauti ya pointi 15 na aliyekuwa akishika nafasi ya pili, Yanga. Wakati huo ligi ikiwa na timu 16 uku kila timum ikicheza michezo 15 kwa kila raundi, Moro ilishindwa kiukusanya pointi 15 tu katika michezo 15 ya mzunguko wa pili, kwaqni Yanga walimaliza mabingwa wakiwa na pointi ambazo hazikuzidi 55, na Moro walikuwa na pointi 40 katika baada ya mzunguko wa kwanza tu, Je, “fitna” ambazo zimekuwa zifanywa na baadhi ya vilabu katika ligi kuu yetu vinaweza kuzuhia matarajio ya Azam FC kama ilivyowahi kutokea kwa timu kama, Pallsons, Moro United?
“Malengo ya mmiliki ni kuifanya klabu ya mfano, Tanzania na Afrika ya Mashariki yote. Hivi sasa ameamua kuwekeza kwa kiasi kikubwa cha pesa, amekamilisha awamu ya kwanza ya ujuenzi wa uwanja wa kisasa, ameamua kuwekeza katika soka la vijana, na uku akichukua wachezaji bora kutoka kila vsehemu anayoweza kufanya hivyo kutokana na mfuko wake ulivyo, tazama hata basi lao, ni la kisasa sana hiyo yote ni kwa sabababu mmiliki anataka timu yake iwe ya mfano na bora bzaidi katika ukanda huu na Afrika, kuhusu kuchukua ubingwa msimu huu? Nadhani wanaweza, ila wanatakiwa watambue ubingwa hauji kwa maneno, bali ni kujiuliza mmejipanga vipi, kuchukua kombe la Mapinduzi ni mafanikio, lakini si kigezo cha kuchukua ubingwa wa ligi kuu, muhimu ni kufanya kazi na kupunga kuongea” anasema kocha huyo, msaidizi wa zamani wa klabu hiyo, Seif King
MATATIZO
Mohammed ambaye anakumbuka kuwa wakati wao wakipanda ligi kuu kulikuwa na ushirikiano mkubwa na umoja ndani ya timu, pamoja na matatizo madogomadogo bado timu iliweza kupanda na kucheza ligi kuu. Mara baada ya kupanda daraja, wachezaji wengi nyota walikuja ndani ya timu hii, mfano ni kama Osborn Monday, Cripsian Odula, Francis Ouma , Ibrahimu Shikanda ambao walikuwa ni wachezaji nyota wa Harambee Stars (timu ya taifa ya Kenya), Danny Wagaruka, Peter SenyondoBen Kalama, ambao walikuwa wachezaji wa Uganda, na wengineo lakini haraka nyota hao waliondolewa baada ya kushindwa kufanya mambo makubwa katika miaska yao ya mwanzo. Ni Ouma pekee ambaye aliuzwa, lakini ni wazi hata Shikanda ataondolewa ndani ya timu hiyo msimu ujao mana hana nafasi.
King ambaye alikuwa sehemu ya benchi la ufundi la timu hiyo kwa muda mrefu anasemaje kuhusiana na tatizo la wachezaji wa kigeni kushindwa kufanya vizuri ndani ya kabu hiyo. “ Ni kweli wachezaji hao walisajiliwa Azam wakiwa na viwango vizuri, nadhani kushindwa kwao kuwika kulitokana na haraka yetu ya kutaka kuona mafanikio ya haraka, kuna baadhi wangeweza kufanya vizuri kama vwangepata muda zaidi, na hilo ndiyo tatizo ambalo limekuwa liliikabili timu hii, wachezaji hawapewi muda wa kuzoea mazingira mapya”
Itamor Amourin aliweza kuwapatia nafasi nwachezaji vijana kama Himid Mao, Abubakary Salum “Sure Boy Jr” na wengineo, lakini pamoja na uwezo mzuri walionao nyota chipukizi ndani ya timu hiyo bado hawajaweza kuaminiwa na kocha wa sasa Stewart Hall, japo ni nyota hao wachanga ndiyo walikuwa sehemu ya timu ambayo ilimaliza katika nafasi ya tatu kwa mara ya kwanza wakiwa na wachezaji wazohefu kama kina Sghekhan, Shaban Kisiga, Salum Sued, Said Sued na wengineo. Azam ilishuhudia timu yao ya vijana ikifanya vizuri mfululizo katika michuano ya Uhai Cup kwa miaka miwili mfululizo na Itamor kuwapatia nafasi baadhi yao katikia timu ya wakubwa. Vijana kama Sino Agustino, Seleman Kassim “Selembe”, Tumba Sued, Jamal Mnyate, Salumu Machaku wote hawa wameanza kucheza ligi kuu wakiwa hapo, hivyo kuna haja ya Azam kuangalia aina yake ya usajili, Je usajili unafanywa na kocha au kuna mtu mwingine nje ya benchi loa ufundi? “ Mpira ni kitaru hivyo Azam wanatakiwa waweke malengo kuwa baada ya muda fulani hatutasajili tena kwa gharama kubwa, kwani watakuwa na yosso wao wanaowazalisha. Usajili watafanya kama sehemu ya kuongeza nguvu sehemu zenye mapungufu, pia wanatakiwa kuywapatia nafasi vijana wao chipukizina wachezaji wakigeni wanaokuwa wakiwasajili” anasema, Mohammed.
Azam inaweza kufanya vizuri na kutimiza lengo walilojiwekea, kwani wanacheza vizuri ndani ya uwanja, lakini kuna muda wa wenyewe, ukifika lazima wakaze “buti” na bukta zao kwani msimu uliopita waliokuwa watatu wakawa wa kwanza, na wa kwanza akamaliza wa tatu.
Friday, March 16, 2012
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Maoni:
Post a Comment