Monday, April 16, 2012

Wasomaji SIB: Azam kuiwakilisha Tanzania

Posted By: kj - 9:56 AM

Share

& Comment


Wasomaji wa mtandao wa mchezo nchini Tanzania Sports In Bongo (SIB) wameipoka ubingwa wa ligi kuu ya Vodacom Yanga SC baada ya kuipa kura nyingi Simba SC na Azam FC kuwa wawakilishi katika michuano inayoandaliwa na shirikisho la soka Afrika CAF mwakani.

Wasomaji na wadau wa SIB waliipa asilimia 64 Simba na Azam, huku Simba na Yanga wakipewa asilimia 30, wakati Yanga na Azam wakipata asilimia 6, kwenye kinyanganyiro cha timu zipi wenye nafasi ya kuiwakilisha Tanzania katika michuano ya CAF mwakani.

Simba SC na Azam FC wamebakisha michezo mitatu huku Yanga akibakisha michezo 4 wakati wakisubiri hatima ya Tibaigana juu ya point zao 3 walizonyanganywa na Kamati ya Ligi, wakiwa nyuma kwa point 10 toka kwa vinara Simba na point 7 toka kwa Azam.


MICHEZO ILIYOSALIA

AZAM FC

Kutokana na rikodi ya Azam FC kutopoteza mchezo pale wanapocheza katika uwanja wake wa Azam uliopo Chamanzi toka wapoteze mbele ya African Lyon katika mchezo wa mwanzoni mwa ligi, unaweza sema hana mchezo mgumu aliobakiza kwani michezo yote anachezea Chamanzi.

AZAM FC Vs MTIBWA SUGAR
Mchezo huu utapigwa April 21, na mara ya mwisho timu hizi kukutana Azam FC wali lala goli 1-0 katika uwanja wa Manungu, hapo mwaka jana, ambapo Mtibwa walizima mwiko wa kufungwa na Azam katika uwanja wa Manungu.

Azam wamekuwa na wakati mgumu pale wanapokabiliana na Mtibwa Sugar nnje ya Manungu na msimu uliopita katika uwanja wa Taifa waliiondoa Azam FC katika kinyanganyiro cha kuwania nafasi ya 2.

AZAM FC Vs TOTO AFRICA
Baada ya kumsimamisha Simba SC katika uwanja wa Taifa na kuvunja mwiko wa kufungwa na Yanga katika uwanja wa CCM Kirumba, April 26 katika uwanja wa Azam Toto Africa watakuwa na dhamira ya kuendelea kuwaduwaza vigogo huku wakijinasua katika janga la kushuka daraja.

Azam FC wamekuwa na wakati mgumu pale wanapo kabiliana na Toto Africa na huu mchezo ndio unaotazamwa kutoa muelekeo wa Azam FC katika kusaka ubingwa wa Tanzania Bara.

AZAM FC Vs KAGERA SUGAR
Mchezo huu utapigwa may 5 katika uwanja wa Azam. Msimu uliopita Azam FC walipoteza point zote 6 kwa Kagera Sugar na msimu huu teyari wamesha poteza point kwao.

Ni mchezo ambao Azam FC wanahitaji kushinda na vilevile Kagera nao, kwa kuwa waweza kuwa katika hatari ya kushuka mpaka watakapo kutana.

SIMBA SC

Vinara Simba wao wamebakisha mchezo 1 mgumu ukiondoa dhidi ya Yanga ambao ni dhidi ya JKT Ruvu katika uwanja wa Taifa.

SIMBA SC Vs JKT RUVU
April 18 inaweza ikarejea yale yaliyotokea msimu uliopita kwa JKT Ruvu kumpotezea dira Simba katika kinyanganyiro cha Ubingwa.

Ugumu wa mchezo huo unatokana na timu zote kuwa na utamaduni wa kuweka chini mpira na ushindi unalalia katikati mwa uwanja.

SIMBA Vs MORO UNITED
Mchezo wa mwisho kabla ya kuwakabili Al ahly shandy utapigwa april 25 katika uwanja wa Taifa.

Mchezo huu unatazamiwa kuwa mrahisi kwa Simba kutokana na rikodi nzuri dhidi ya Moro united, ila mambo yanaweza kuwa tofauti kutokana na mahali Moro united alipo.

YANGA SC

Yanga amebakisha michezo miwili migumu huku wakitamani warejeshewe point 3 na Tibaigana. Michezo yenyewe ni dhidi ya Kagera Sugar na JKT Oljoro.

KAGERA SUGAR Vs YANGA
April 18 katika uwanja wa Kaitaba ndipo Yanga atakapo juwa hatima yake katika kutetea ubingwa kama Tibaigana hato warejeshea yanga point 3 zao.

Endapo Yanga akipoteza mchezo huo atakuwa amejitoa katika kinyanganyiro cha ubingwa. Na huwa na wakati mgumu katika uwanja wa Kaitaba japo kuwa Kagera Sugar hawako vizuri msimu huu.

YANGA Vs POLISI DODOMA
Mchezo huu utakao chezwa Taifa april 22, hautarajiwi kuwa mgumu kwa Yanga. Polisi Dodoma yupo mkiani mwa ligi.

YANGA Vs OLJORO
JKT Oljoro wamekuwa hawatabiliki katika duru la pili, na huwa wa gumu katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid ambapo Yanga watakaribishwa april 25.

SIMBA Vs YANGA
Mchezo huo wa watani wajadi utapigwa mei 5 katika uwanja wa Taifa, ambapo uzito wake utategemeana na matokeo ya michezo iliyosalia kabla ya kufunga ligi kwa kukutana.

Mchezo huo unaweza ukawapa ubingwa Azam FC kama watachanga vyema karata zao 3.

0 Maoni:

Post a Comment

Copyright © CHAMA LANGU NI AZAM FC™ is a registered trademark.

Designed by Templateism. Hosted on Blogger Platform.