Thursday, May 3, 2012

Azam kuwakabili wakatamiwa wikend hii

Posted By: azam fans - 10:01 PM

Share

& Comment


Mabingwa wa kombe la Mapinduzi Azam FC itakwaana na wakatamiwa wa Kagera na katika mashamba ya Manungu, Kagera Sugar na Mtibwa Sugar ndani ya siku 3 michezo ya ligi kuu ya Vodacom.

Azam FC kesho (ijumaa mei 4) saa kumi alasiri katika uwanja wa Taifa watawavaa Mtibwa Sugar kufuatia matokeo ya mchezo wa awali ulioshindwa kukamilika kufutwa.

Kamati ya nidhamu na usuluhishi iliyochini ya Alfreid Tibaigana iliamuru mchezo huo uliochezwa katika uwanja wa Azam urudiwe kabla ya michezo ya mwisho, hivyo kusegezwa mbele kwa siku moja michezo yote ya mwisho ya ligi kuu ya vodacom.

Baada ya mchezo huo Azam FC watashuka katika uwanja wake wa Azam kuwakaribisha Kagera Sugar siku ya jumapili katika mchezo wa kufunga msimu wa ligi kuu ya vodacom.

Azam FC wanaitaji ushindi katika michezo yote miwili na wanaitaji kukusanya tofauti ya magoli 5 ya kufunga na kufungwa katika michezo hiyo na kuiombe Simba SC wapoteze mchezo wao dhidi ya yanga ili kuipa nafasi kwa mara ya kwanza kutwa wazwa mabingwa wa Tanzania Bara.

0 Maoni:

Post a Comment

Copyright © CHAMA LANGU NI AZAM FC™ is a registered trademark.

Designed by Templateism. Hosted on Blogger Platform.