Saturday, May 5, 2012

Azam kushiriki kombe la shirikisho CAF

Posted By: azam fans - 12:06 PM

Share

& Comment

Mabingwa wa Mapinduzi Azam FC sasa watashiriki michuano ya kombe la shirikisho CAF mwakani, baada ya jana kupoteza mchezo kwa Mtibwa Sugar na kuwaacha Simba watwae ubingwa wa Tanzania Bara.

Katika mchezo wa jana Azam FC walipoteza nafasi kadhaa za kujipatia magoli, huku wakicheza soka lao la kutambaza mpira chini.

Mtibwa Sugar walio kuwa wakishangiliwa kwa nguvu dakika zote za mchezo toka katika jukwaa linalo kaliwa na mashabiki wa Simba katika uwanja wa Taifa waliandika goli la kwanza katika dakika ya 25 kupitia kwa Awadh Issa akiunga kona ya Juma Abdul.

Juma Abdul aliipatia Mtibwa Sugar goli la pili kwa mpira wa adhabu iliyosababishwa na beki Luckson Kakolaki baada ya kumkwatua Vicent Barnabas katika dakika ya 59.

Goli pekee la waakilishi wa Tanzania katika michuano ya kombe la shirikisho Mwakani, Azam FC lilifungwa na John Raphael Bocco na kufikisha magoli 18 katika michezo ya ligi kuu ya vodacom na magoli 23 msimu huu.

0 Maoni:

Post a Comment

Copyright © CHAMA LANGU NI AZAM FC™ is a registered trademark.

Designed by Templateism. Hosted on Blogger Platform.