Monday, May 7, 2012

AZAM YAANZA SAFARI MPYA NA MALENGO MAPYA

Posted By: azam fans - 1:08 AM

Share

& Comment


Salum Abubakary Sure Boy

Mabingwa wa Mapinduzi Azam FC wameanza safari mpya hapo jana katika ukumbi JB Bel Monte uliopo Benjamin Mkapa Tower.

Azam FC walioshika nafasi ya pili katika msimu wa Ligi kuu ya Vodacom, katika kuelekea kwenye kilele cha safari mpya kuna malengo wamejiwekea hapo jana ambayo ni kutwa ubingwa wa Tanzania Bara na kufanya vyema katika mashindano ya kimataifa.

Katika tafrija ya kuwaga msimu wa 2011/12 na kuweka wazi nini wanakitarajia katika safari yao mpya kulikuwa na wageni mbalimbali, akiwemo mwenyekiti wa Simba Muheshimiwa Ismail Aden Rage, Mbunge wa Kinondoni Muheshimiwa Iddi Azan na wageni wengineo.

Kocha Stewart Hall alisema katika tafrija hiyo kuwa "Next job to be come number one" akimaanisha kazi iliyombele yake ni kuhakikisha Azam FC inachukua nafasi ya kwanza msimu ujao na kutwawazwa mabingwa wa Tanzania Bara.

Vilevile katibu mkuu wa TFF Angetile Osiah alipewa fursa ya kuzungumza kwa niaba ya TFF na kusema kuwaondoa Celtic na Ranger lazima uwe na mbinu za kutosha zenye kueleweka akilenga kuzipoteza Simba na Yanga, kwani Celtic na Ranger ndio wanaopokezana kuchukua ubingwa wa Scotlanda.

Isamael Aden Rage alipo pewa nafasi ya kuzungumza alisema anaiombea Azam iweze kukalia nafasi ya pili wala si ubingwa kwani ukiondoa Mtibwa Sugar, timu nyingine zilizo subutu kuchukuwa ubingwa zilikufa, hivyo haitakii Azam kifo ndio maana haitakii ubingwa.

Katika Tafrija hiyo wachezaji wa Azam FC na Azam Academy walipatiwa tuzo mbalimbali, pamoja na waandishi wa habari za michezo na vyombo vya habari.

WALIOPATA TUZO TOKA KWA AZAM FC

Mchezaji Bora: John Raphael Bocco
Mchezaji asiyechuja (outstanding player): Salum Abubakari 'Sure Boy'
Mchezaji Anayekuja juu (most promising player): Khamisi Mcha Viali
Mchezaji Muhamasishaji: Aggrey Morrise
Mchezaji mwenye nidhamu ndani na nnje ya uwanja: Waziri Salum
Motivation Player: Ibrahim Shikanda
Mchezaji mtiifu mazoezini: Lackson Kakolaki
Mchezaji mchangamfu: Erasto Nyoni
Mchezaji aliyefiti msimu mzima: Said Morad.

0 Maoni:

Post a Comment

Copyright © CHAMA LANGU NI AZAM FC™ is a registered trademark.

Designed by Templateism. Hosted on Blogger Platform.