Friday, June 15, 2012

Aggrey ambwaga Kaseja kwenye Tuzo za TASWA

Posted By: kj - 6:14 AM

Share

& Comment


Nahodha wa Azam FC, Aggrey Morise jana usiku aliongeza idadi ya tuzo kabatini mwake ikiwa ni miezi miwili imepita toka uongozi wa Azam FC umpatie tuzo ya mchezaji muhamasishaji ndani ya klabu.

Aggrey jana alipokea tuzo ya mchezaji bora wa mpira wa miguu nchini katika mwaka wa 2011/12, na kuwabwaga kipa wa Simba SC, Juma Kaseja na mfungaji bora wa wakati wote wa Azam FC John Raphael Bocco katika kinyanganyiro hicho.

Aggrey ambaye ni nahodha msaidizi katika kikosi cha Kim Poulsein ameisadia Azam FC kutwa kombe la Mapinduzi pamoja na kuiwezesha Azam FC kushika nafasi ya pili katika msimamo wa ligi kuu ya Vodacom.

Wachezaji wengine wa Azam FC waliokuwa katika Tuzo hizo zilizotolewa na Chama cha Waandishi wa Habari za michezo TASWA zilishuhudia wachezaji wengine wa Azam FC wakizidiwa kete na wachezaji wa Simba SC.

Katika kipengele cha mchezaji bora wa kigeni nchini, mshambuliaji wa Azam FC Kipre Tchetche alipigwa chini na Mganda Emanuel Okwi aliyepata tuzo hiyo.

Sure Boy Jr (Salum Abubakari) alitoka patupu kwa Shomari Kapombe katika kipengele cha mchezaji bora Chipukizi, na Kapombe ndiye aliyetwaa tuzo ya mwanamichezo bora wa mwaka 2011.

Kwa niaba ya Azam FC Fans Club twampa hongera nahodha wetu Aggrey na tunawapongeza Sure Boy na Tchetche kwa kuweza kuteuliwa katika kinyanganyiro hicho.

0 Maoni:

Post a Comment

Copyright © CHAMA LANGU NI AZAM FC™ is a registered trademark.

Designed by Templateism. Hosted on Blogger Platform.