Tuesday, June 12, 2012

Azam waanzia gym jana

Posted By: azam fans - 6:42 AM

Share

& Comment



KIKOSI cha timu ya Azam kimeanza mazoezi ya viungo 'Gym' jana kujiandaa na michuano ya Kombe la Kagame inayotarajiwa kuanza baadaye mwezi huu.

Afisa habari wa timu hiyo Jaffar Iddi, alisema wachezaji wote wamewasili kambini na tayari wameeanza mazoezi ya viungo kwa ajili ya kuweka viungo sawa kabla ya kuanza mazoezi ya uwanjani.

"Wachezaji wote wamefika na wameanza mazoezi sambamba na kocha wao mkuu Stewart Hall," alisema Jaffar.

Akizungumzia mikakati yao kuhusu michuano ya Kombe la Kagame, Jaffar alisema bado wamejipanga kuhakikisha wanatwaa ubingwa huo.

Azam wamemaliza msimu wa Ligi Kuu uliopita na kushika nafasi ya pili pia ni mabingwa wa michuano ya Kombe la Mapinduzi.


SOURCE: MWANANCHI

0 Maoni:

Post a Comment

Copyright © CHAMA LANGU NI AZAM FC™ is a registered trademark.

Designed by Templateism. Hosted on Blogger Platform.