Baada ya kuwa mapumzikoni kwa takribani mwezi mmoja, wachezaji wa Azam FC wameanza kuwasili jijini Dar es Salaam kwa maandalizi ya kushiriki mashindano ya klabu bingwa Afrika Mashariki na Kati (CECAFA).
Kulingana na program ya maandalizi, Azam FC wataanza mazoezi June 8, Ijumaa hii maalum kwa mashindano hayo yatakayo fanyika nchini mwezi ujao.
Hii ni mara ya kwanza kwa Azam FC kushiriki mashindano hayo ikiwa imepata nafasi hiyo baada ya kumaliza msimu uliopita wa 2011-2012 kwa kushika nafasi ya pili, nafsi hiyo inawapa pia nafasi nyingine ya kushiriki Kombe la Shrikisho kwa nchi za Afrika litakalianza Januari mwakani.
Wachezaji wa kutoka nje ya Tanzania watawasili mapema wiki hii kwa maandalizi ya makazi kabla ya kuanza kwa mazoezi hayo yatakayofanyika kwenye uwanja wa Azam Chamazi.
Kambi ya Azam FC itaathiriwa kidogo na kambi za timu za taifa ambapo baadhi ya wachezaji wamo kwenye timu hizo, wachezaji waliopo kwenye timu za taifa ni Joseph Owino (Uganda Cranes) George Odhiambo (Kenya) Aggrey Morris, Mwadini Ally, Deogratius Munishi, Erasto Nyoni, Waziri Salum, Salum Abubakar, Mrisho Ngasa, na John Bocco (Taifa Stars - Tanzania). na Abdulhalim Humud, Khamis Mcha, Abdi Kassim na Abdulghani Ghulam Abdallah (Zanzibar heroes) iliyoenda kucheza kombe la dunia la mataifa yasiyo wanachama wa FIFA na hapo juzi iliibajua Ratia 6-0 Khamis Mcha akifunga magoli matatu peke yake.
Usajili kwa wachezaji ulifamalizika kabla ya wachezaji kwenda likizo hivyo wachezaji wote waliosajili wataanza mazoezi isipokuwa wale waliokuwa kwenye timu za Taifa (Tanzania, Taifa Stars, Uganda ‘The Cranes na Zanzibar Heroes) ambao watajiunga na wenzao baada ya kumaliza michezo inayowakabili.
Programu ya maandalizi ya CECAFA itamalizika siku moja kabla ya kuanza mashindano hayo mwezi ujao, mashindano yatakapomalizika timu itakuwa na mapumziko ya siku chache kabla ya kuanza maandalizi kwa ajili ya ligi kuu ya Vodacom (VPL) msimu ujao wa 2012-2013.
Maandalizi kwa ajili ya VPL yataenda sambamba na kambi kwa wachezaji pamoja na safari ya kujiandaa na msimu huo ‘Pre- season tour’ itakayofanyika nchi itakayotajwa baadae.
Wachezaji wote wataungana na wapya waliosajili msimu huu ambao ni George ‘Blackberry’ Odhiambo kutoka Kenya na kipa Deogratius Munishi watajiunga wachezaji waliotoka Azam Academy ambao ni AishiSalum, Juckson Wandwi, Dizana, Ibrahim Rajab Jeba na Joseph Kimwaga.
Kikosi kamali cha Azam FC kinaundwa na Magolikipa, Mwadini Ally, Deo Munishi "Dida" Aishi Salum na Jackson Wandwi
Mabeki wa Pembeni upande wa kulia Ibrahim Shikanda na Erasto Nyoni, kushoto ni Waziri Salum na Samih Haji Nuhu
Mabeki wa kati ni Luckson Kakolaki, Said Moradi, Joseph Owino na Aggrey Morris
Viongo ni Kipre Bolou, Abdulhalim Humud, Himid Mao, Salum Abubakar, Abdi Kassim Sadala, Ramadhani Selemani Chombo, Abdulghani Ghulam, Ibrahim Rajab Jeba, Jabir Aziz Stima, na Ibrahim Joel Mwaipopo.
Washambuliaji wa pembeni ni Kipre Tchetche, Mrisho Ngasa, Zahoro Pazi, Khamis Mcha, na George Odhiambo "Blackberry".
Washambuliaji wa kati ni Gaudence Mwaikimba na John Bocco
0 Maoni:
Post a Comment