Sunday, July 1, 2012

Azam FC timu yenye nidhamu

Posted By: kj - 7:08 AM

Share

& Comment


Mabingwa wa Mapinduzi Azam FC wametwaa tuzo ya timu yenye nidhamu bora katika msimu wa 2011/12 wa ligi kuu ya vodacom, huku tuza za mchezaji bora, kocha bora na mfungaji bora zikitoa Azam FC.

Katika hafla ya utoaji wa tuzo hizo uliofanyika katika hoteli ya Double Tree By Hilton, huku mgeni rasmi akiwa Waziri Mkuu mstaafu Fredirick Sumaye, tuzo ya kipa bora alichukua Juma Kaseja toka Simba SC.

Frank Domayo aliyejiunga yanga akitokea JKT Ruvu, Rashid Mandawa wa Coastal Union na Hasan Dilungwa wa Ruvu Shooting, walitwaa tuzo mpya ya mchezaji toka kikosi B aliyepandishwa kwenda kikosi A na kufanya vyema. Tuzo hiyo ilitambulishwa na katibu mkuu wa TFF Angetile Osiah.

Nahodha wa Azam FC na mchezaji muhamasishaji Aggrey Morice alibeba tuzo za mchezaji bora wa msimu huo wa ligi kuu, huku kocha wake Stewart Hall akichukua tuzo ya kocha bora wa msimu.

Kinara wa mabao wa Azam FC John Raphael Bocco 'Adebayor' alijiondokea na tuzo ya mfungaji bora wa msimu wa 2011/12 wa ligi kuu ya vodacom.

0 Maoni:

Post a Comment

Copyright © CHAMA LANGU NI AZAM FC™ is a registered trademark.

Designed by Templateism. Hosted on Blogger Platform.