Saturday, July 21, 2012

Azam watoa suluhu na Tusker, watinga robo Kagame

Posted By: kj - 6:01 PM

Share

& Comment

Mabingwa wa kombe la Mapinduzi Azam FC leo mchana wamefanikiwa kutinga hatua ya robo fainali ya kombe la Kagame baada ya kutoka suluhu na Tusker ya Kenya mchezo uliochezwa katika uwanja wa Taifa.

Katika mchezo huo Tusker walilazimika kumaliza pungufu, baada ya kipa wao Boniphace Olouch kuzawadiwa kadi nyekundu na mwamuzi Issa Kagabo kwa kumchezea rafu John Bocco 'Adbayor' wakati anakwenda kufunga katika dakia ya 51.

Azam FC hii leo walicheza mchezo wataratibu na katika kipindi cha kwanza eneo la kati la uwanja lilimilikiwa na Tusker kabla ya kulirudisha katika himaya yao katika kipindi cha pili, huku Azam FC wakipoteza nafasi kadhaa za kuandika goli.

Azam FC na Mafunzo ndizo zilizotinga hatua ya robo toka katika kundi B lililokuwa na timu 3, wakati timu zote zikimaliza na point 2, hivyo Azam FC na Mafunzo wanatinga hatua hiyo kutokana na kuwa na goli 1 ambapo Tusker hawana goli lolote lile la kufunga baada ya kutoka suluhu ya bila kufungana na AZam FC pamoja na Mafunzo.


Azam FC leo; Deo Munishi ‘Dida’, Aggrey Morris, Erasto Nyoni, Ibrahim Shikanda, Jospeh Owino, Kipre Ballou, Kipre Tchetche/Mrisho Ngassa, Ibrahim Mwaipopo, John Bocco/Gaudence Mwaikimba, Ramadhan Chombo na Hamisi Mcha ‘Vialli’.

0 Maoni:

Post a Comment

Copyright © CHAMA LANGU NI AZAM FC™ is a registered trademark.

Designed by Templateism. Hosted on Blogger Platform.