Mchezaji bora wa Azam FC ameongeza uhasama kwa mashabiki wa Simba baada ya kuwafanya watoke kimya kimya uwanja wataifa hii leo, katika mchezo wa robo fainali ya 4 ya kombe la Kagame na kuipeleka Azam FC nusu fainali ambapo watacheza na AS Vita hapo alhamisi katika dimba la Taifa.
Katika mchezo huo ulioanza saa kumi alasiri, Azam FC waliuwanza mchezo vyeme kwa kulitawala eneo la kati ya uwanja lililo kuwa chini ya Salim Abobakari, akisaidiwa na Ibrahim Mwaipopo na Ramadhan Chombo.
Simba nusura wapate goli katika dakika ya 8 lakini uimara wa kipa mpya wa Azam FC Deo Munich 'Dida' alizuia hatari hiyo. Katika dakika ya 17 Salum Abubakari alimchopea Ibrahim Shikanda ambaye alipiga krosi iliyoungwa kwa kichwa na John Raphael Bocco na mpira kutinga katika nyavu za Juma Kaseja.
Kuingia kwa goli hilo lilizidisha utawala wa Azam FC katika sehemu ya kiungo na kuwapoteza kabisa viungo vya Simba, na kupelekea timu kwenda mapimziko Azam wakiwa mbele kwa goli 1-0.
Azam FC walirejea na kasi waliyomalizia kipindi cha kwanza na dakika ya 46 John Raphael Bocco alirejea kwenye nyavu za Kaseja na kuiandikia Azam goli la pili, na kuzidi kuipoteza Simba huku mashabiki wa Simba wakikaa kimya.
Shomari Kapombe alikuja kuisawazishia Simba katika dakika ya 53, goli lililo rudisha Simba mchezoni kabla ya Bocco kufunga goli lake la 4 la mashindano likiwa la 3 katika mchezo huo kwake katika dakika ya 73 na kuzima ndoto za Simba kutinga hatua ya nusu fainali.
Hadi kipenga cha mwisho kinapulizwa Azam 3-1 Simba, hivyo Azam watacheza na AS Vita ya DR Congo siku ya Al hamisi katika uwanja wa Taif. baada ya AS Vita kuichapa Atletico goli 2-1 katika mchezo uliochezwa saa 8 mchana.
Azam FC leo: Deo Munish, Ibrahim Shikanda, Erasto nyoni, Aggrey Morice, Said Morad, Ibrahim Mwaipopo, Salum Aboubakari, Ramadhan Chombo, Khamis Mcha/Jabir Azizi, John Bocco, Kipre Tchetche/Odhiambo

0 Maoni:
Post a Comment