John Bocco alipowalambisha ice cream za Azam Simba hapo jana |
Mfungaji bora wa ligi kuu ya Vodacom msimu uliopita, John Raphael Bocco jana jioni aliwasha indicator ya kusaka ufungaji bora wa kombe la kagame, wakati akiendelea kumnyanyasa na kuwa mtanzania pekee aliyeziona nyavu za Tanzania one Juma Kaseja mara nyingi.
Juma Kaseja ambaye anaaminikia kuwa ni Tanzania One (Chaguo la Kwanza langoni) kwa kipindi hiki cha miaka 10, amefungwa na John Bocco 'Adbayor' magoli 14, baada ya magoli matatu aliyofunga katika mchezo wa jana.
John Bocco 'JB19' ameziona nyavu za Simba na Yanga mara 23 katika michezo 28 aliyocheza dhidi ya timu hizo kongwe na zenye upinzani wa jadi nchini, akiwa kaifunga Simba SC goli 14 katika michezo 15 na Yanga magoli 9 katika michezo 13 aliyocheza.
Mchezaji Bora wa mwaka wa klabu ya Azam FC John Bocco ameifungia Azam FC jumla ya magoli 53 katika michezo 62 aliyoichezea Azam katika ligi kuu ya Vodacom, toka apande na timu hiyo toka ligi daraja la kwanza.
Katika msimu wake wa kwanza ligi kuu ya Vodacom (2008/09) alifunga magoli 8, na msimu wa 2009/10 na 2010/11 amefunga magoli 13, huku msimu uliopita (2011/12) akiziona nyavu mara 19 na kutwaa kiatu cha dhahabu.
Imeandaliwa kwa msaada wa meneja wa Azam FC Patrick Kahemele
0 Maoni:
Post a Comment