CALVIN KIWIA
KIUNGO nyota wa Azam FC, Salum Aboubakary 'Sure Boy', alimfunika Haruna Niyonzima 'Fabregas' wa Yanga kwa pasi nyingi wakati wa mechi ya fainali ya Kombe la Kagame iliyochezwa wikiendi iliyopita.
Sure Boy alitoa idadi kubwa ya pasi katika mchezo huo na kufuata nyayo za baba yake, Aboubakary Salum ambaye katika miaka ya nyuma aliwahi kung'ara kwenye michuano hiyo.
Baba yake huyo ambaye naye aliitwa Sure Boy, alikuwa winga wa zamani wa Yanga ambaye alitikisa kwenye mashindano ya mwaka 1986, ambayo pia yalifanyika jijini Dar es Salaam.
Nyota ya Sure Boy imetamba katika fainali na kurudia mafanikio ya baba yake ambaye katika fainali ya mwaka huo aliisaidia kuisawazishia Yanga mabao mawili na kufanya ifungane 2-2 na El-Merreikh ya Sudan.
Kitendo hicho Aboubakary cha kufunga mabao mawili katika dakika za mwisho za mchezo huo kilifanya apewe jina la 'Sure Boy' na mtangazaji maarufu wa zamani wa Redio Tanzania, Charles Hillary. El-Merreikh, hata hivyo, ilishinda kwa penalti 6-4 na kutwaa kombe.
Kwa Sure Boy wa sasa, naye timu yake ilichapwa (2-0) na Yanga iliyotwaa kombe.
Sure Boy alitoa pasi nyingi katika mchezo ule baada ya kugawa pasi 71 ambapo 55 ziliwafikia watu lakini pasi 16 zilikwenda fyongo.
Niyonzima, ambaye hakutoa pasi iliyozaa bao licha ya timu yake kushinda, alipiga jumla ya pasi 36 wakati 32 ziliwafikia walengwa na nne hazikuwapata watu.
Kwa upande wa krosi, Niyonzima ndiye alitamba katika eneo hilo wakati alipiga mbili na Sure Boy hakupiga hata moja.
Nyota hawa licha ya kusifika kuchezesha timu zao pia wanajulikana kwa mashuti na Niyonzima alipiga matatu huku moja likilenga golini lakini mwenzake alipiga mawili na yote yalitoka nje.

0 Maoni:
Post a Comment