Azam FC leo wamefanikiwa kutinga hatua ya nusu fainali ya kombe la BankABC Super8 baada ya kuwachapa goli 2-1 maafande wa Morogoro 'Polisi Moro'.
Katika mchezo huo Polisi walikuwa wa mwanzo kupata goli katika dakika ya kwanza, kabla ya beki kisiki Said Morad kusawazisha katika dakika ya 20, huku kiungo Abdi Kassim Babi 'Balack wa Unguja' kuifungia Azam goli la Ushindi.
Kwa ushindi huo Azam FC watacheza na Simba SC katika nusu fainali ya pili itakayochezwa saa 10 alasiri agosti 15 mwaka huu katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam, huku ya kwanza ikiwakutanisha Mtibwa sugar na Jamhuri SC.
Michuano hiyo inataraji kufikia tamati hapo agosti 18.
Katika hatua nyingine Mfungaji bora wa klabu John Raphael Bocco amesha kwenda nchini Afrika Kusini kwa ajili yamajaribio ya siku 7 katika timu ya Super sport.
Azam Fans Club inawatakia kila la kheri JB 19 katika majaribio yake iliaweze kufuzu na kufungua njia kwa wengine.
0 Maoni:
Post a Comment