Friday, September 21, 2012

AZAM KUWAKABILI WAKATAMIWA

Posted By: kj - 10:53 PM

Share

& Comment

Baada ya kumaliza michezo ya kanda ya Ziwa, Azam FC kesho wanateremka kwa mara ya kwanza katika msimu wa 2012/13 katika uwanja wa Azam kuwakaribisha wakatamiwa wa Manungu, Mtibwa Sugar.

Azam FC inashuka katika mchezo huo ikiwa na kumbukumbu ya kutoka na sare na Toto African katika mchezo wa mwisho wa ligi, wakati wapinzake wake Mtibwa Sugar wakitokea katika ushindi wa goli 3-0 walio upata mbele ya Yanga.

Katika michezo mitatu ya mwisho iliyowakutanisha Mtibwa Sugar na Azam FC, ilishuhudia ushindi ukielekea kwa wakatamiwa wa Manungu Mtibwa Sugar.

Azam FC chini ya kocha mpya Boca imempatia nafasi kiungo chipukizi Himid Mao Makame kuendelea kuonyesha uwezo wake huku jukumu la kuichezesha timu likiwa kwa kiungo Abdulhalim Homoud ambaye atapambana vilivyo na kiungo mkongwe Shaban Kisiga.

Mtibwa na Azam wote wanapoint 4 lakini Mtibwa Sugar akimzidi Azam tofauti ya magoli ya kufunga na kufungwa ambapo Mtibwa Sugar wanamagoli 3 na Azam wana 1.

0 Maoni:

Post a Comment

Copyright © CHAMA LANGU NI AZAM FC™ is a registered trademark.

Designed by Templateism. Hosted on Blogger Platform.