ABOODMSUNI NETWORK inawaomba radhi mashabiki wa Azam FC wanaopendelea kutembelea katika kurasa ya livescore na ratiba katika blog ya Azam Fans Club ambao utoa matokeo ya Azam na michezo mingine ya ligi kuu moja kwa moja toka viwanja.
ABOODMSUNI NETWORK ndiyo inayoendesha ukurasa huo wakiiunga kutoka katika ukurasa wa dakika 90 ndani ya Sports In Bongo.
Katika mchezo wa jana kurasa hiyo ya Azam Fans Club ilikuwa inachelewa kutoa taarifa na kupelekea kusimama katika dakika za mwanzo wa kipindi cha pili.
Matatizo hayo yalisababishwa na majaribio ya Aboodmsuni Network katika kusaka namna bora ya kuwasilisha matokeo ya moja kwa moja.
Kutokana na hilo Aboodmsuni Network ilikuwa inajaribu hiyo platform mpya ambayo imeonekana imeshindwa kazi na tumeamua kurejesha ile ya awali. Na nimatumaini yetu mambo yatakuwa sawa katika michezo ya jumamosi.
Imetolewa na ABDALLAH H.I SULAYMAN
mmiliki wa ABOODMSUNI NETWORK
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Maoni:
Post a Comment