Monday, September 3, 2012

MKATABA WA REDONDO WAUZWA SIMBA KWA MIL25

Posted By: azam fans - 9:44 PM

Share

& Comment

Azam FC imefikia uwamuzi wa kumuachia kiungo mchezeshaji Ramadhani Chombo 'Redondo' kujiunga na Simba SC, baada ya Simba SC kukubalia kutoa shilingi milion 25 kununua mkataba wa Redondo.

Mseamaji wa Azam FC Jafari Iddi Maganga amesema kuwa Simba SC wamekubalia kutoa kitita hicho cha pesa kwa awamu, ambapo wametanguliza milioni 10 na 15 zingine zitakamilika katika mchezo wa ngao ya jamii.

Kutokana na kufikia maelewano hayo Azam FC wanatarajia kufuta pingamizi walilo liweka kupinga Redondo kujumushwa katika usajili wa Simba SC wakati akiwa na mkataba na Azam FC, hivyo Redondo kuwa huru kukipiga na Simba SC.

0 Maoni:

Post a Comment

Copyright © CHAMA LANGU NI AZAM FC™ is a registered trademark.

Designed by Templateism. Hosted on Blogger Platform.