Thursday, September 27, 2012

TUKUTANE TAIFA TUHESABU PASI

Posted By: kj - 5:14 PM

Share

& Comment

Ukitaka burudani ya kuhesabu pasi katika soka la bongo, basi usikubali kupitwa na mchezo unao wakutanisha Azam FC na JKT Ruvu, ambapo kesho wanakutana katika uwanja wa Taifa katika muendelezo wa mzunguko wa nne wa ligi kuu ya vodacom.

Mchezo huo utakao anza saa moja kamili usiku katika dimba la Taifa hapo kesho (september 28) utaonyeshwa moja kwa moja na kituo cha Super sport 9 na kutangazwa katika masafa ya Kissfm, huku blog yako ya Azam Fans ikishindwa kukuletea mtanange huo moja kwa moja kupitia ukurasa wa Livescore & Ratiba, kutokana na mwendesha kurasa hiyo 'ABOODMSUNI' kwa wakati huo kukamatwa na shughuli iliyompeleka Morogoro.

Aboodmsuni yupo Morogoro toka Alhamisi ya wiki jana akiweka mambo sawa ambapo anatarajiwa kukamilisha siku ya jumamosi na kurejea Dar es salaam kuendeleza gwaradumu la livescore katika blog za Azam Fans Club na Sports In Bongo.

Azam FC kesho itashuka uwanjani ikiwa na kumbukumbu ya kutopoteza mchezo tangu ligi kuu ya vodacom ianze hapo september 15 na endapo ikishinda hapo kesho itakwaa kwa mara nyingine katika usukani wa Ligi ambao kwa sasa inashikiliwa na Simba SC.

Wakati JKT Ruvu wakiwa wamepoteza michezo miwili mpaka sasa na kuruhusu nyavu zao kuguswa mara 7 wao wakigusa nyavu za wapinzani mara 3, wakiwa wameshinda mchezo mmoja.

Pamoja na JKT Ruvu kucheza mchezo unao endana na Azam FC, Azam FC wamekuwa na kazi rahisi kupata ushindi kila inapokutana nao, na huenda kesho John Bocco akarejea katika utikisaji nyavu baada ya kutoka bila ya goli katika michezo mitatu iliyopita.

Kipre Michael Bolou huenda akaanza baada ya kuingia akitokea benchi katika mchezo dhidi ya Mtibwa Sugar ikiwa ndio urejeo wake toka aumie katika mchezo wa robo fainali kombe la Kagame dhidi ya Simba SC, huku wadau na mashabiki wakingoja urejeo wa Salum Abubakari 'Sure Boy' ambaye ajacheza mchezo wowote wa ligi zaidi ya ule wa ngao ya jamii dhidi ya Simba SC akitokea benchi.

Kikosi chote cha Azam FC kiko vizuri huku kiungo chipukizi Himid Mao akizidi kurejea kwa kasi baada ya kupotea msimu uliopita sambamba na beki Samih Haji Nuhu.

Viingilio Katika mchezo huo ni sh. 3,000 mzunguko, sh. 5,000 kwa VIP C na VIP B wakati VIP A kiingilio kitakuwa sh. 10,000.

0 Maoni:

Post a Comment

Copyright © CHAMA LANGU NI AZAM FC™ is a registered trademark.

Designed by Templateism. Hosted on Blogger Platform.