Saturday, October 6, 2012

AZAM WAIPUMULIA SIMBA, BOCCO AFUNGUA MBIO

Posted By: kj - 6:51 PM

Share

& Comment


Alikuwa mfungaji bora wa wakati wote wa klabu ya Azam FC John Raphael Bocco akifunga goli lake la pili kwa msimu huu na kuifanya Azam FC kufikisha point 13 sawa na vinara Simba SC wakizidiwa goli moja.

Azam FC leo iliwakaribisha African Lyon katika uwanja wa Azam uliopo Chamanzi, na Kocha Boca akitumia kikosi kile kile kilicho anza dhidi ya Ruvu shooting na kufanikiwa kutoka na ushindi wa goli 1-0.

Ilibidi mashabiki wa vikundi vya Mpira kazi toka Magomeni na wale wa Majimatitu na wengineo waliojitokeza Uwanjani hapo dakika 45 kushuhudia goli pekee katika mchezo lililofungwa na John Raphael Bocco.

Katika kipindi cha Pili Azam FC walifanya mabadiliko ya Kutoka Ibrahim Mwaipopo na nafasi yake kuchukuliwa Salum Abubakary (Sure Boy) na Gaudence Mwaikimba akichukuwa nafasi ya Kipre Tchetche, mabadiliko hayo hayakubadili matokeo.

Katika dakika ya 87 Azam FC walipata pigo baada ya beki wake wa kushoto Samih Hajji Nuhu kuzawadiwa kadi nyekundu na mwamuzi Israel Majuna Nkongo.

0 Maoni:

Post a Comment

Copyright © CHAMA LANGU NI AZAM FC™ is a registered trademark.

Designed by Templateism. Hosted on Blogger Platform.