Friday, October 5, 2012

GOLI TATU KUTUWEKA KILELENI MWA LIGI

Posted By: kj - 8:26 PM

Share

& Comment

Mabingwa wa Mapinduzi na washindi wa pili wa ligi kuu ya vodacom 2011/12 Azam FC kesho watawakaribisha timu yenye bifu na waendesha soka nchini TFF, African Lyon katika uwanja wa Azam, mpambano wa ligi kuu ya vodacom.

Azam FC ambayo imeshuka uwanjani mara 4 bila kupoteza mchezo wowote, wakiwa wametoa sare mchezo mmoja na kushinda mitatu, wataitaji kushinda goli 3-0, ili warejee tena kileleni mwa ligi.

Simba SC inayoongoza ligi wakiwa wameteremka uwanja mara 5 wamewazidi Azam FC point 3 na tofauti ya magoli mawili ya kufunga na kufungwa.

Kikosi cha Azam FC kipo vizuri teyari kwa mpambano huo wa kesho (oktobar 6) dhidi ya African lyon na huenda wakaendelea kumkosa kiungo Abdulhalim Homoud aliyeifungia Azam FC goli 2.

Mpaka sasa Kipre Tchetche ndie aliyeifungia magoli mengi Azam FC akiwa amefunga goli 3 huku John Raphael Bocco akiwa amefungua ukurasa wake katika mchezo uliopita kwa kuifungia Azam FC goli moja sawa na Kipre Bolou aliyeifungia Azam FC katika mchezo huo.

0 Maoni:

Post a Comment

Copyright © CHAMA LANGU NI AZAM FC™ is a registered trademark.

Designed by Templateism. Hosted on Blogger Platform.