Monday, April 22, 2013

AZAM NA COASTAL KUCHEZWA APRIL 26, AZAM KWENDA MOROCO APRIL 28

Posted By: Unknown - 7:34 PM

Share

& Comment

Mchezo wa ligi kuu ya vodacom kati ya Coastal union na Azam fc utachezwa april 26 mwaka huu badala ya aprili 27 katika uwanja wa Mkwakwani mkoani Tanga.

Mchezo huo umerudishwa siku moja ilikuipa fursa Azam kujiandaa kwa mechi ya marudiano ya kombe la shirikisho dhidi ya AS FAR Rabat ya Moroco.

Mechi hiyo itachezeshwa na Andrew Shamba kutoka Pwani akisaidiwa na Abdallah Mkomwa wa Pwani na Vicent Mlabu wa Morogoro, wakati mwamuzi wa mezani atakuwa Mohamed Mkono wa Tanga na Charles Komba wa Dodoma atakuwa Kamishna.

Baada ya mechi Azam itarejea Dar es Salaam siku inayofuata tayari kwasafari yakwenda Rabat april 28 wakati mechi yao itachezwa kati mei 3 ,4 na 5 mwaka huu.

0 Maoni:

Post a Comment

Copyright © CHAMA LANGU NI AZAM FC™ is a registered trademark.

Designed by Templateism. Hosted on Blogger Platform.