Monday, April 22, 2013

AZAM NA RABAT WAINGIZA MIL 50

Posted By: Unknown - 7:49 PM

Share

& Comment

Mech ya kwanza ya Raundi ya tatu ya Kombe la shirikisho kati ya Azam fc na AS FAR Rabat uliochezwa juzi (april 20 mwaka huu) imeingiza Sh.
50,850,000.

Fedha hizo katika mechi hiyo iliyochezwa katika Uwanja wa Taifa na kumalizika kwa timu hizo kutoka suluhu zimetokana na watazamaji 8,268 waliokata tiketi.

Viingilio vilikuwa sh. 5,000 sh 10,000, sh 15,000, sh 20,000 na sh 30,000.

Mgawo ulikuwa kama ifuatavyo; gharama za tiketi sh.
5,575,500, asilimia 15 ya uwanja sh. 6,791,175, asilimia 10
ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) na Shirikisho la Soka Afrika (CAF) sh. 4,527,450 na asilimia 75 iliyokwenda kwa klabu ya Azam ni sh. 33,955,875.

0 Maoni:

Post a Comment

Copyright © CHAMA LANGU NI AZAM FC™ is a registered trademark.

Designed by Templateism. Hosted on Blogger Platform.