Saturday, April 27, 2013

STAR TV KUONYESHA MCHEZO KATI YA AZAM NA WAMOROCO

Posted By: Unknown - 10:25 AM

Share

& Comment

Mchezo wa marejeano hatua ya tatu kombe la shirikisho baina ya wakilishi pekee wa Tanzania, Azam FC na AS FAR Rabat ya Moroco utakao chezwa mei 4 nchini Moroco utaonyeshwa moja kwa mnja kupitia Star tv.

Star tv ambao wamekuwa wakionyesha michezo mbalimbali ya azam fc kupitia udhamini wa bidhaa zizalishazo na SSB, sambamba vituo vya redio vinavyo milikiwa na Sahara Communication Kiss fm na radio free Afrika masafa ya kati watakuwa moja kwa moja toka Moroco siku hiyo ya mpambano.

"Mchezo Kati ya Azam FC na AS FAR utakaochezwa nchini Morocco jumamosi tarehe 4/5/2013 utarushwa live na Star TV," ilieleza taarifa ya azam fc katika ukurasa wao wa jamii (facebook).

Katika mchezo huo azam fc watakuwa na kibarua cha kusaka ushindi ama kutoa sare ya magoli ili wapate nafasi ya kutinga hatua inayofuata.

Azam fc wanataraji kuondoka kesho jumapili (aprili 28) kwenda Moroco na kikosi kizima kilicho sajiliwa na azam fc kwa ajili ya michuano hiyo ya kimataifa.

Mashabiki mbalimbali wamekuwa wakiuliza je Aggrey Morise, Erasto Nyoni, Saidi Morad na kipa Deo Munish ni miongoni mwa wachezaji watakau kuwemo katika msafara huo?

Mpaka sasa bado sijapata jawabu toka kwa viongozi wa azam fc lakini kulingana na moja ya taarifa walizowahi kutoa huko nyuma wakati timu ikijiandaa kwenda Liceria ambayo inasema wachezaji wote 25 waliosajiliwa kwa ajili ya michuano hiyo ukiwaondoa wachezaji watatu ambao ni Jackson Wandwi, Omari Mtaki na Samih Hajji Nuhu ndio watakao kosa safari hiyo.

0 Maoni:

Post a Comment

Copyright © CHAMA LANGU NI AZAM FC™ is a registered trademark.

Designed by Templateism. Hosted on Blogger Platform.