Friday, April 26, 2013

AZAM WATOKA SARE NA COASTAL UNION

Posted By: azam fans - 7:24 PM

Share

& Comment

Azam fc leo wametoka sare ya goli 1-1 na Coastal union ya Tanga katika mchezo wa kuwania ubingwa wa Tanzania bara ambao teyari Yanga wamesha utwaa.

Mchezo huo uliochezwa katika uwanja wa Mkwakwani ulishuhudia kocha Stewart Hall akiwapa nafasi mabeki Erasto Nyoni na Aggrey Morise waliokuwa nnje ya kikosi cha azam fc kwa takribani miezi 5 huku akiwapumzisha Waziri Salum, Jackson Atudo, Khamis Mcha, Michael Bolou, Kipre Tchetche na Salum Aboubakari aliyeingia kipindi cha pili.

Katika kipindi cha kwanza ambacho kilimalizika kwa sare ya bila kufungana kila timu ilicheza kwa kujihami na kupeleka mashambulizi kadhaa ambayo yaliishia kwa walinda milango Shaban Kado upande wa Coastal na Mwadini Ally kwa azam fc.

Kipindi cha pili kilianza kama cha kwanza kilivyokuwa kabla ya mabadiliko yaliyofanywa katika kila pande kuongeza kasi ya mchezo.

Katika dakika ya 57 mshambuliaji wa azam fc Gaudence Mwaikimba aliangushwa na Ibrahim Yusuph Chuma katika eneo la hatari na mwamuzi kuamuru penati iliyotiwa kimiani na Aggrey Morise.

Mabadiliko ya kumuingiza Daniel Liyanga kuchukua nafasi ya Selemani Kasim Selembe katika dakika ya 68 ilizaa matunda baada ya Liyanga kuisawazishia goli Costal union katika dakika ya 70, na kupelekea mchezo kumalizika kwa sare 1-1.

Azam fc leo: MWADINI ALLY, HIMID MAO, ERASTO NYONI, AGGREY MORICE, DAVID MWANTIKA, IBRAHIM MWAIPOPO, BRIAN UMONY, JABIR AZIZI, GAUDENCY MWAIKIMBA, HUMPHREY MIENO NA JOHN BOCCO.

0 Maoni:

Post a Comment

Copyright © CHAMA LANGU NI AZAM FC™ is a registered trademark.

Designed by Templateism. Hosted on Blogger Platform.