Barack YC II itatua Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) saa 3.35 asubuhi kwa ndege ya PrecisionAir ikitokea Nairobi, Kenya inapounganisha safari hiyo inayoanzia Monrovia kupitia Accra, Ghana.
Msafara wa timu hiyo utakuwa na watu 37 wakiwemo wachezaji 21 na utaongozwa na Ofisa Mtendaji Mkuu (CEO) wa klabu hiyo, Robert Alvin Sirleaf ambaye ni mtoto wa Rais wa Liberia, Ellen Johnson Sirleaf.
Azam fc na Barack YCwatakutana katika mchezo wa marejeano utakao fanyika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam siku ya jumamosi april 6, baada ya ule wa awali uliochezwa katika mji wa Monrovia nchini Liberia na kumalizika kwa azam fc kuibuka na ushindi wa goli 2-1.
Azam wanahitaji sare ya aina yoyote ile ili waende kwenye hatua nyingine ambayo watakutana kati ya timu toka Morocco ama AL Nasri ya Libya.
--
MSUNI COMPUTER SOLUTION (Tunarejesha uhai wa computer)
www.aboodmsuni21.blogspot.com/p/msuni-computer-solution_7934.html
0 Maoni:
Post a Comment