Sunday, March 31, 2013

AZAM WAPUNGUZA POINT KWA YANGA

Posted By: azam fans - 11:47 AM

Share

& Comment

Wawakilishi wa Tanzania waliosalia katika michuano inayoandaliwa na CAF katika ngazi xa vilabu Azam fc jana walipunguza tofauti ya point baina yao yanga kufuatia ushindi walio upata huku yanga wakitoa sare na polisi morogoro.

Azam fc walikuwa katika uwanja ambao kwao kupata ushindi huwa si kazi rahisi, uwanja wa Mabatini Kibaha kuwakabili wenyeji wao Ruvu shooting ukiwa ni muendelezo wa michezo ya ligi kuu ya vodacom iliyochezwa hapo jana.

Pamoja na mchezo huo kuonyeshwa moja kwa moja 'live' kupitia star tv, lakini umati mkubwa wamashabiki ulijitokeza na kuvunja rikodi ya uwanja huo, ambao simba na yanga hawaendi kucheza michezo yao ya ugenini dhidi ya ruvu shooting.

Azam fc iliyotawala vyema eneo la kati lililokuwa chini ya Michael Bolou na Salum Aboubakari walipata goli la kuongoza katika dakika ya 44 kupitia kwa Kipre Herman Tchetche akifunga goli lake la 14 msimu huu wa 2012/13 na kuweka mazingira mazuri ya kubakisha kiatu cha dhahabu ndani ya azam fc ambapo msimu uliopita alichukua John Bocco.

Endapo Kipre akifanikiwa kuibuka mfungaji bora, utakuwa ni mwaka wa 3 mfufululizo azam fc inatoa mfungaji bora baada ya Mrisho Ngassa akiwa azam katika msimu wake wa kwanza (2010/2011) aliibuka mfungaji bora, mfungaji bora wawakati wote wa Azam fc alifanya hivyo katika msimu wa 2011/12 na sasa Muivory coast Kipre Tchetche anaongoza kwa kuziona nyavu.

Ubora wa safu ya ulinzi ya azam ilikuwa chini ya kipa chipukizi Aishi Manuel, beki Himid Mao, Waziri Salum, Lukson Kakolaki na Joackins Atudo ulipelekea Ruvu shooting kushindwa kupata goli huku John Bocco akipoteza nafasi kadhaa na kupelekea mchezo kwisha kwa azam kutoka na ushindi wa goli 1-0.


MATOKEO MENGINE YA VPL HAPO JANA.

POLISI MORO 0-0 YANGA
KAGERA SUGAR 3-1 MTIBWA SUGAR
TOTO AFRICA 2-2 SIMBA
AFRICAN LYON 1-0 COASTAL UNION
--
MSUNI COMPUTER SOLUTION (Tunarejesha uhai wa computer)
www.aboodmsuni21.blogspot.com/p/msuni-computer-solution_7934.html

0 Maoni:

Post a Comment

Copyright © CHAMA LANGU NI AZAM FC™ is a registered trademark.

Designed by Templateism. Hosted on Blogger Platform.