Saturday, June 29, 2013

AZAM KUWEKA KAMBI AFRIKA KUSINI

Posted By: Unknown - 11:12 PM

Share

& Comment

Mabingwa wa kombe la muungano mara mbili mfululizo Azam FC wamepanga kwenda kuweka kambi nchini Afrika Kusini kwa ajili ya maandalizi ya msimu ujao unao tarajiwa kuanza mwezi wa nane mwaka huu.

Azam Fc ambayo wameanza mazoezi ya kujiwinda na msimu ujao wa ligi kuu ya Tanzania Bara inayo dhaminiwa na vodacom tangu juni 24 mwaka huu wanataraji kwenda Afrika kusini hapo baadae kwa ajili ya michezo kadhaa ya kujipima nguvu kabla ya msimu ujaanza.

Msimu ulio isha Azam FC walitembelea Kenya kwa ajili ya michezo ya kirafiki ambapo ziara yao hiyo na ile ya katikati ya msimu ya nchini DR Congo katika jimbo la Kinshasa yaliiwezesha Azam FC kupata nafasi ya kushiriki kombe la shirikisho kwa mara nyingine tena hapo mwakani.

Azam FC inaendelea na mazoezi yao katika uwanja wa Azam Complexs bila ya nyota wake waliopo timu ya Taifa na wachezaji wake wa wili wakulipwa toka Ivory coast Kipre Bolou na Kipre Tcheche.

Kikosi cha Azam FC kinatarajiwa kukamilika julai mosi kwa wachezaji wote kuwasili. Na ikumbuke kuwa Azam FC hawaja ongeza sura mpa katika kikosi chao zaidi ya kuwapandisha wachezaji watatu toka kikosi cha pili cha Azam FC (Azam academy)

0 Maoni:

Post a Comment

Copyright © CHAMA LANGU NI AZAM FC™ is a registered trademark.

Designed by Templateism. Hosted on Blogger Platform.