Saturday, October 5, 2013

AZAM WATOA SARE NA COASTAL, KIPRE AKIPIGWA NA CHUPA

Posted By: azam fans - 7:31 PM

Share

& Comment

Azam fc leo wameendelea kukusanya pointi moja baada ya kutoka sare ya bila kufungana na Coastal union katika mchezo uloshuhudia urushwaji wa chupa na mawe uwanjani.
Katika mchezo huo wa saba wa ligi kuu ya vodacom uliochezwa katika uwanja wa Mkwakwani timu zilikuwa zinashambuliana kwa zamu.
Katika dakika 42 mwamuzi msaidizi (mshika kibendera) alirushiwa jiwe na kupelekea mchezo kusimama kwa takribani dakika 3 mpaka 4.
Katika kipindi cha pili timu ziliendelea kushambuliana kwa zamu na mnamo dakika 65 John Raphael Bocco alikwamisha mpira nyavuni na mwamuzi kulikataa goli kwa madai yalifanyika madhambi kabla ya mpira kumfikia Bocco.
Dakika 5 mbele beki wa Coastal union alizawadia kadi nyekundu na dakika 3 mbele Kipre Tcheche alimanusura aipatia Azam fc goli la kungoza lakini mpira wa Abdallah Seif Karihe uliyomkuta katika 6 aliupaisha.
Baada ya kosa hilo Kipre Tcheche alirushiwa chupa na mashabiki waliojitokeza katika uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga.
Hadi dakika 90 zinakamilika Azam fc na Coastal union wakitoa sare ya bila kufungana na timu zote mbili wakifikisha pointi 11 wakiwa nyuma kwa pointi 4 toka kwa vinara simba sc.

AZAM FC LEO: MWADINI ALLY, ERASTO NYONI, WAZIRI SALUM, AGGREY MORISE, SAID MORAD, KIPRE BOLOU, BRIAN UMONYI/ABDALLAH SEIF, SALUM ABOUBAKARI, JOHN BOCCO, HUMPHREY MIENO NA KIPRE TCHECHE.





0 Maoni:

Post a Comment

Copyright © CHAMA LANGU NI AZAM FC™ is a registered trademark.

Designed by Templateism. Hosted on Blogger Platform.