Tuesday, October 29, 2013

TCHECHE AIPA AZAM UONGOZI WA LIGI

Posted By: Unknown - 3:29 AM

Share

& Comment

Magoli mawili ya mshambuliaji wa Ivory coast Kipre Herman Tcheche yalitosheleza kuipatia Azam FC point tatu muhiu na kujikita katika kilele cha msimao wa ligi kuu ya vodacom kwa kufikisha point 23.

Azam FC leo waliwakabilia Simba sc katika mchezo wa ligi kuu ya vodacom uliochezwa katika uwanja wa taifa jijini Dar es salaaam, na Azam FC kufanikiwa kuwa timu ya kwanza kufunga Simba SC katika msimu huu wa ligi kuu ya vodacom.

Simba SC ndiyo waliokuwa wa mwanzo kupata goli kupitia kwa Ramadhani Singano ‘Messi’ aliyemalizia mpira ulioingizwa kutoka pembeni na Zahor Pazi katika dakika ya 21.

Azam walisawazisha goli hilo katika dakika ya 43 kupitia kwa Kipre Herman Tchetche aliyemalizia mpira wa Erasto Nyoni kutoka pembeni kulia, na kupelekea timu kwenda mapumziko wakiwa sare ya goli 1-1.

Azam FC walianza kipindi cha pili, kwa kufanya mabadiliko ambapo Joseph Kimwaga alitoka na kumpisha Faridi Mussa Maliki katika dakika ya 47, mabadiliko ambayo yaliongeza kasi ya mchezo huku wakishambuliana kwa zamu.

Kipre Herman Tcheche aliyekuwa mfungaji bora wa msimu uliopita, alimfungisha tera William Lucian ‘Gallas’ kisha kumchambua Abbel Dhaira kwa ustadi wa hali ya juu na kuandika goli la pili kwa azam FC na kupelekea mchezo kumalizika kwa Azam FC kuibuka na ushindi wa goli 2-1.

Kikosi cha Azam FC leo kilikuwa; Mwadini Ally, Erasto Nyoni, Waziri Salum, Aggrey Morris, Said Mourad/David Mwantika dk47, Kipre Balou, Kipre Tchetche, Salum Abubakar ‘Sure Boy’, John Bocco, Humphrey Mieno/Khamis Mcha dk 73 na Joseph Kimwaga/Farid Mussa dk47.

0 Maoni:

Post a Comment

Copyright © CHAMA LANGU NI AZAM FC™ is a registered trademark.

Designed by Templateism. Hosted on Blogger Platform.