Friday, January 10, 2014

AZAM FC WAACHIA UBINGWA WA MAPINDUZI

Posted By: Unknown - 7:00 PM

Share

& Comment

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgRITRxT6nPEaSjdU-xlps4U8HHy3pvjMDSNhklxaJO2gihx2Iyqu2nK4xGbFMSXp3MQKvEwOPbB-yot-nrgnrbmj0JUAGAPf2gxTKa6YFGcg_BwlsptndrP8ikpGVYspVJNoUaPzAr8gY/s1600/1492260_687549097952116_1204020894_o.jpg

Mabingwa watetezi wa Kombe la Mapinduzi, Azam wameutema ubingwa huo baada ya kukubali kipigo cha magoli matatu 3-2 katika mchezo wa kwanza wa nusu fainali uliopigwa uwanja wa Amaan Zanzibar.

Wakati ikionekana kama kwamba mchezo ulikuwa ukielekea katika changamoto ya mikwaju ya penati huku magoli yakiwa 2-2 KCC waliandika goli la tatu na la ushindi katika ya 90 kupitia kwa William Wadri kwa mkwanju wa chinichini akiwa pembeni kushoto mwa lango la Azam nje kidogo ya eneo la hatari na kumuacha mlinda lango Ally Mwadini akiduwaa.

Mwadini alikuwa ametoka kumzuia mfungaji baada ya kuwaona walinzi Erasto Nyoni akizidiwa mbio na Wadri na hivyo kuliacha lango wazi na jitihada za walinzi wawili wa kati; Davidi Mwantika na Aggrey Morris kuzuia mpira uliompita Mwadini hazikufua dafu.

Azam watajilaumu wenyewe kwani walikuwa wa kwanza kufunga mabao mawili ya kuongoza katika dakika za 17 na 31 kupitia kwa mshambuliaji kinda Joseph Kimwaga, kwanza kwa kichwa akiunganisha mpira wa kona iliyochongwa na Erasto Nyoni na baada akiunganisha vema pasi ya chini chini ya Kipre Tchetche.

Waganda hawakukata tama na kufanikiwa kurejesha matumaini ya kutinga fainali kwa kujipatia goli la kwanza kwa kichwa likitiwa kimiani na Ibrahim Kiiza kwa kichwa akiunganisha mpira wa adhabu ndogo ulipigwa na Habib Kavuma, katika dakika ya 37.

KCC waliendeleza pale walipomalizia kipindi cha kwanza kwani walifanikiwa kusawzisha katika dakika ya 51 mfungaji Tony Odur akiunganisha pasi ya chinichini ya Kavuma aliyemshinda mbio Erasto nyoni.

Kwa ujumla kipindi cha pili kilikuwa tofauti kabisa kwani KCC walitawala mchezo huku wakionekana kukimbia kwa kasi na kuwalazimisha wachezaji wa Azam na hasa safu za ulinzi na kiungo kufanya makosa mongi hadi pale waganda walipofanikiwa kupata goli la ushindi katika dakika 90.

Katika mchezo huo mshambuliaji kinda wa Azam Joseph Kimwaga ametangazwa mchezaji bora wa mchezo na kuzawadiwa kisimbuzi cha Azam TV, utaratibu ambao umekuwepo kuanzia hatua ya robo fainali.

Kwa matokeo hayo Azam ambao walikuwa wametwaa Kombe la Mapinduzi mara mbili mfululizo wamelitema rasmi na kuliachia likiwaniwa na KCC ambao wapo fainali pamoja na Simba na URA ya Uganda, timu mbili zitakazokutana usiku huu katika nusu fainali ya pili.

0 Maoni:

Post a Comment

Copyright © CHAMA LANGU NI AZAM FC™ is a registered trademark.

Designed by Templateism. Hosted on Blogger Platform.